Askofu
Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God hapa nchini Dk.Moses
Kulola (pichani), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa
za kifo cha askofu huyu maarufu zimetolewa na mtoto wake Mwiinjilisti
Daniel Kulola ambaye ameitoa kupitia mtandao wa face book ambapo
ameueleza umma wa watanzania kuwa baba yake mzazi amefariki dunia katika
hospitari ya Aga Khan ambako alikuwa amelazwa.
Hajaeleza
marehemu alikua anaumwa nini lakini taarifa zinasema amekuwa mgonjwa
siku nyingi ambapo aliwahi kulazwa nje ya nchi na baadae akarudishwa
nchini na hatimae kufariki Dunia.
Hadi
hivi sasa haijajulikana askofu kulola atazikwa lini lakini pia taarifa
zimethibitishwa rasmi kutoka kwa wachungaji mbalimbali ambao wako chini
ya kanisa lake ambalo lina mtandao nchi nzima na lenye waumini zaidi ya
milioni 5 nchini kote.
Moses
Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na
watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka
1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga
na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la
AIC Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na wamezaa watoto 10 ambapo saba bado hai.
Alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi
serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji.
Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua
kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964
alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuan makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila. Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake.
Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana
anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia
yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa
kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito
mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60
amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana,
katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani
jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana
kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola na injili iliyonyooka na
akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa
milele bure.MUNGU ambariki sana mtumishi wake huyu ni mfano hai kwa
watumishi wa MUNGU wa sasa
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe
No comments:
Post a Comment