Tangazo

August 26, 2013

JK AZINDUA BARAZA LA USHAURI LA WASTAAFU WA CCM, AONGOZA KIKAO CHA NEC DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda viwanja vya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo kuzindua Baraza la Ushauri la Viongozi wastaafu wa CCM. nyuma ya Kinana ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), wakishangilia wakati wa hafla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuzindua Baraza hilo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alipowasili kwenye uzinduzi wa Baraza hilo. Mwinyi baadaye alichagulia na wanabaraza wenzake kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza hilo Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM (Bara) John Malecela na watatu kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimakribisha Rais Kikwete kuzindua Baraza la Ushauri la Viongozi wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma. Wengine  kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Bara) John Malecela, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Rais Mstaafu Ali Hassan Miwnyi na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kutoka kulia (walioketi) ni Makamu Mwenyekitin wa CCM mstaafu (Bara) Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM (Zanzibar), Dk. Amani Abeid Karume na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakay6a Kikwete akizindua Baraza la Ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, leo mjini Dodoma, huku akiwa na wajumbe wa baraza hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza kabla ya kuzindua baraza hilo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ana Makamu wake (Zanzibar) Dk. Ali Mohammed Shein wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, baada ya kuzindua baraza hilo leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Kinana.
 Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Viongozi wastaafu wa CCM, Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongoza kikao cha kwanza cha Baraza hilo leo mjini Dodoma. Kushoto ni Wajumbe wa Baraza hilo John Malecela na Amani Abeid Karume na kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Benjamin Mkapa na Katibu wa Baraza Pius Msekwa.
 Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao chca NEC kilichofanyika leo mjini Dodoma kama Baraza la Kitaifa la Kitaasisi kujadili maoni ya rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na mabaraza ya chini ya kitaasisi ya CCM hivu karibuni. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Sheni na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wajumbe wa Baraza la Ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, Kutoka kulia, John Malecela, Amani Abeid Karume na Pius Msekwa wakiwa kwenye kikao cha NEC, baada ya Baraza hilo kualikwa kwa ajili ya kushiriki katika mjadala wa rasimu ya Katiba mpya kwa upande wa CCM kama taasisi.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasilisha makusanyo ya maoni ya katiba kama yaliyotolewa na mabaraza ya ngazi za chini ya CCM kama taasisi, leo kwenye kikao hicho cha NEC.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana mambo na watendaji wenzake katika Chama, nje ya ukumbi wa White House mjini Dodoma leo, kabla ya kuzinduliwa Baraza la Ushauri la Wastaafu wa CCM . Kutoka kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhamed Seif Khatib, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo.
 Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimshauri Jambo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa Baraza la ushsuri la Wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma.
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika uzinduzi wa Baraza hilo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia mmoja wa wana-CCM waliohudhuria hafla ya kuzinduliwa Baraza la Washauri la Wastaafu wa CCM leo mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Hamis akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Martine Shigela wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye akiwa katika ukumbi wakati wa kikao cha NEC leo mjini Dodoma

Katibu wa NEC, Itrikadi na uenezi Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu yaliyojiri katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika jana. Pamoja na mambo mengine, Nape amesema, Kamati Kuu amejadili suala ya sakata la madiwani wanane katika Halmashauri ya Bukoba, mkoani Kagera ambao Halmashauri Kuu ya CCM mkoa huo ilitangaza kuwatimua hivi karibuni ambapo Nape amesema, Kamati Kuu imeamua kuwaita ili kukutana nao kesho viongozi wanane katika mkoa huo aliowataja kuwa Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini, Mbunge wa Bukoba mjini na Meya wa Halmashauri ya Bukoba. IMETAYARISHWA NA BASHIR NKOROMO

No comments: