Tangazo

September 2, 2013

Frank Filman ateuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Kitengo cha Teknolojia IT cha Airtel Tanzania.

Airtel Tanzania inatangaza uteuzi wa Bw. Frank Filman (pichani), kuwa mkurugenzi wa kitengo cha teknolojia ya IT aliyechukua nafasi hiyo rasmi kuanzia
sasa

Filman ambaye ni mtanzania alianza kazi Airtel akiwa kama munagalizi wa system (system Admistrator) na baadaye alipanda cheo na kuwa Meneja wa Mradi wa Technolojia ya IT. Kutoka mwaka 2007 mpaka 2009, alikuwa Meneja wa kitengo hicho nchini Ghana ambapo alisimamia na kutoa mchango mkubwa  uzinduzi wa mtandao wa Airtel  nchini Ghana.

Mwishoni mwa mwaka 2009 Filman alirejea Tanzania akiwa kama Meneja wa Huduma za kimtandao  (Network service Manager ) za Airtel Tanzania.

Baadaye alijiunga na kitengo cha mauzo na kama meneja wa Techonologia na biashara na huko aliweza kuchangia ongezeko la mapato kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 100%  kwa mienzi 12 tu.

Katika miaka yake 12 na Airtel, Filman amefanya kazi miaka miwili Airtel Ghana na zaidi ya miaka tisa akiwa na Airtel Tanzania.

Akizungumzia juu ya uteuzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema "Uteuzi wa Filman kuwa Mkurugenzi wa kitengo cha Teknolojia ya IT ni ushahidi wa dhamira ya Airtel Tanzania kuendeleza, kulea na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake ndani ya nchi.

Sisi tunayo furaha kubwa kuona Watanzania wanachukua majukumu makubwa katika moja ya makampuni yanayokuwa kwa kasi na nyeti kama hii.Teknolojia ya IT ni msingi muhimu wa mafanikio katika mawasiliano ya simu kwa sababu huduma zetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na  huduma za kifedha yaani Airtel Money na  internet zinategemea teknolojia hiyo."

Aliendelea kwa kusema Kampuni imemteua Bw. Filman ikiwa na uhakika kwamba ataifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kabisa.

"Tunaamini Bw. Filman atafanya vyema kazi yake kutokana na uzoefu alionao lakini vilevile Airtel itaendeleza dhamira yake kuwaendeleza na kuwawezesha wafanyakazi wengine kushika nyazifa kama hizi nchini na kwenye nchi nyingine za Afrika na Asia ambapo Airtel inafanya biashara. pia Airtel tutaendelea kuwapa mafunzo wafanyakazi wetu ambayo yatawafanya wawe kwenye viwango vya kimataifa" Alisema Bw. Golaso.

Akizungumzia uteuzi wake Filman alisema, "Nimekuwa nikitamani kupata nafasi hii na nilijua siku moja naweza nikaipata na ninayofuraha kupata wadhifa huu Airtel Tanzania . kwa miaka mingi nimepitia mafunzo mbalimbali, na nina uzoefu nilioupata nchini Ghana pamoja na nchi nyingine Airtel inayofanya biashara. Hivyo niko tayari na nimejiandaa vyema kukabiliana na changamoto zote katika utendaji wa kazi hii na kuhakikisha natoa huduma zenye ubora kwa watanzania."

Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara.  Airtel imewekeza katika kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa alisema bw Sunil Colaso mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania.

Airtel imeweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha wafanyakazi wa Airtel wanatoa huduma bora za kitaalamu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kumekuwa na fursa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wafanyakazi wa Airtel Tanzania katika vitengo vya masoko, Mauzo, IT, pamoja na kuwa na mfumo wa kuwapeleka baadhi ya wafanyakazi wake nchi tofauti kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa kufanya kazi kwa mienzi 6 hadi 18 katika Airtel Afrika na India.

Airtel pia imekuwa ikiendesha mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wa mauzo, masoko na huduma kwa Wateja kupitia Chuo Kikuu cha Centum .

Ambapo wafanyakazi wamekuwa wakipewa ujuzi na maarifa muhimu yanayowasaidia kutoa huduma bora kwa wateja ambazo zinaleta maendeleo makubwa na kuonesha utofauti katika soko la ushindani la mawasiliano ya simu.

No comments: