Tangazo

September 2, 2013

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE REDDS MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2013!

Happiness Watimanywa
Na Mwandishi wetu.

Mrembo wa Mkoa wa Dodoma,  na mwakilishi wa Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji la Redds Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa  mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2013.

Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.

Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka magazeti ya Serkali Daily News, Habarileo na Spotileo.

Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha wa Jambo Leo Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.

Dalili za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa kwashangwe.

Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness Watimanywa aliyeibuka mshindi.

Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.

Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.

Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa.

Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar es Salaam Septemba 21,2013.


 Mrembo huyo ambaye pia anashikilia taji la Miss Dodoma 2013 na Miss Kanda ya Kati 2013, ana digrii ya Biashara aliyoipata kupitia chuo cha Strathclyde University cha UK na aliwahi kuwa wa kwanza na kuongoza nchi zipatazo 150 katika somo la Accounts kwa shule zinazofanya mtandao wa IGCSE, Happiness alikuwa akisoma katika shule ya Saint Constantines International School ya Arusha. Alivumbuliwa na kipindi maarufu cha wanafunzi SKONGA kinachooneshwa kupitia televisheni ya EATV na kuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengi nchini Tanzania na kwingineko.

No comments: