Tangazo

October 2, 2013

MAX KOMBA NA PENDO WALIVYOMEREMETA KATIKA HARUSI YAO

Harusi hii ya aina yake,  imefungwa Jumaosi, Septemba 28, 2018, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelo, Kigango cha Tabata, Dar es Salaam, na baadaye mnuso mkali ukafanyika katika Hoteli ya Serena (zamani kabisa ikiitwa Sheraton Hotel' katikati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania. Bwana harusi, Max ambaye ni mwenyeji wa Ruvuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kizalendo ya Kotes Tanzania Ltd, huku Bibi Harusi Mrs Pendo Komba akiwa ni mwenyeji wa katikati ya Tanzania, mkoa wa Dodoma. Picha tulipiga nyingi sana! lakini kwa kuwakilisha hapa zipo picha 200, Karibu.
Bwana Max Komba
Mrs Pendo Max Komba
Pendo wakati akiwa bado humo katika shera
Baadhi ya wageni kutoka Ruvuma wakigaragara chini kama ishara ya kumheshimu Bwana Komba, walipowasili nyumbani kwa Bwana harusi, Tabata Dar es Salaam, tayari kushiriki suguli nzima ya harusi iyo.
Komba akiwa mbele ya nyumba yake, muda mfupi kabla ya kwenda Kanisani.
Wageni wakipata chakula cha mchana nyumbani kwa Komba.
Mapishi yakiendelea kabla ya watu kwenda harusini.
Mmoja wa wapambe wa karibu akimsauri jambo Komba kabla ya kwenda kufunga ndoa.
Baadhi ya waalikwa wakiwa katika basi maalum kwenda Kanisani.
Na awa pia.
Komba akitoka rasmi nyumbani kwenda Kanisani kufunga ndoa.
Komba na mpambe wake wakiwasili kanisani, gari hili alilotumia siyo la kukodi, ni mali yake.
Padre akampokea Komba na mpambe wake.
Shamrashamra zikiendelea kanisani kupokea maharusi.
Bi Pendo ambaye sasa ni Mrs Komba akiwasili Kanisani.
Pendo akiingia kanisani.
Komba na mkewe wakiwa mbele ya Padre.
Hapa wakiwa tayari kufungishwa ndoa
Na hapa pia.
Wakisubiri kwa hamu kufumgishwa ndoa.
Padre akiwa mbele yao kuwaleza mambo muhimu yahusuyo ndoa...
Baadhi ya watoto wanafamilia, ndugu na jamaa wakiwa kanisani.
Kwaya ya kanisa ikisherehesha kwa nyimbo za mapambio.
Baadhi ya wazee wa karibu wa bwana harusi.
waalikwa wakiwa kanisani.
Maharusi na wapambe wao wakiwa kanisani.
Kisha padre akaja mbele yao.
'Shikaneni mikono' Padre akasema, nao wakafanya hivyo.
Na Padre akaweka mkoni wake juu ya mikono yao kuwafungisha ndoa.
Ikawa kama ivi...Picha kibao zaidi, tafadhali BOFYA HAPA

No comments: