Msanii Mrisho Mpoto akielezea kupitia mashairi
Mama Zaida Mgalla akitoa ufafanuzi kwa ripota wa Uwezo TV Bi. Melania Mhagama
Mgeni Rasmi akionyesha ripoti baada ya kuzindua.
Wakati
ambapo asilimia 100 ya watoto wa Darasa la 3 na kuendelea wanapaswa kuweza
kusoma na kufanya hesabu za kiwango fulani, matokeo ya Uwezo yanaonyesha kwamba
ni wachache tu ndiyo wanaoweza kufanya hivyo.
Katika
Darasa la 3, mmoja kati ya watoto wanne anaweza kusoma Kiswahili kwa kiwango
sahihi. Shule za binafsi zinafanya vizuri zaidi kidogo kulinganisha na zile za
Serikali, ambapo asilimia 61 ya watoto walio na umri chini ya miaka 9 hawawezi kusoma
Kiswahili na kufanya Hesabu za Kuzidisha kulinganisha na asilimia 85 ya wenzao
walio katika shule za Serikali.
Matokeo
haya yalitangazwa na Twaweza, inayosimamia Tafiti ya Uwezo, katika ripoti yake
ya tatu ya Tathmini ya Mwaka ya Ujifunzaji. Matokeo haya yamejikita zaidi
kwenye tathmini kubwa kabisa ya mwaka kwa ngazi ya kaya inayopima stadi za
kusoma na kufanya hesabu za msingi za watoto.
Tathmini
ilifanyika nchi nzima mwaka 2012; ikipima watoto 104,568 wenye umri kati ya
miaka 7 hadi 16 katika kaya 55,191, katika maeneo (vijiji) 3,752, kwenye wilaya
126 za Tanzania.
Tathmini
ya Uwezo inaonyesha kwamba utendaji uko duni nchini kote. Matokeo muhimu
yalikuwa:
Stadi ya kusoma Kiswahili –
Matokeo bado ni duni na hayajabadilika sana tangu 2011Mtoto 1 tu kati ya 4 (26%) wa Darasa la 3 anaweza kusoma
hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.
Kwa
Darasa la 7, mtoto 1 kati ya 4 (24%) bado hakuweza kusoma hadithi ya ngazi ya
Darasa la 2.
Stadi ya kusoma Kiingereza –
Matokeo yalikuwa mabaya zaidi kuliko katika Kiswahili
Katika
Darasa la 3, 1 tu kati ya watoto 10 (13%) aliweza kusoma hadithi ya ngazi ya
Darasa la 2.
Hata
katika Darasa la 7, ni watoto 5 kati ya 10 walioweza kusoma hadithi ya ngazi ya
Darasa la 2.
Kufanya hesabu –
Matokeo yamepanda zaidi kuliko mwaka 2011 lakini bado ni duni
Katika
Darasa la 3, zaidi kidogo ya watoto 4 tu kati ya 10 (44%) walioweza kufanya
Hesabu za kuzidisha.
Kufika
Darasa la 7, mtoto 1 tu kati ya 10 (11%) aliweza kufanya Hesabu ya ngazi ya
Darasa la 2.
Matokeo
haya yanaonyesha kwamba kundi kubwa kabisa la watoto halipati ujuzi muhimu
katika elimu ya msingi. Hata wanapomaliza elimu ya msingi, watoto bado
wanashindwa kufanya zoezi la ngazi ya Darasa la 2.
Kuna tofauti kubwa nchini:
Tathmini
ya Uwezo inaonyesha jinsi tofauti ya kimatabaka inavyozidi kukua. Watoto katika
maeneo ya mijini wanafanya vizuri zaidi kuliko wenzao wa vijijini katika
masuala ya kusoma na kuandika.
Watoto wanaotoka
kwenye kaya zenye kipato cha juu vilevile walionekana kufanya vema zaidi katika
stadi hizi za msingi, sawa sawa na watoto wanaosoma katika shule za binafsi.
Ingawa matokeo ya kujifunza kwa ujumla wake ni duni, tofauti hizi zinazozidi
kukua zinaonyesha kuwa mfumo wa elimu unawanufaisha zaidi wale wenye hali bora.
Watoto wote, bila kujali umri, darasa au hadhi
ya shule walijaribiwa kwa kutumia ngazi ya kusoma na kufanya hesabu ya Darasa
la 2. Matokeo muhimu yalikuwa:
Mahali Katika umri wa miaka 9, ni watoto 3 tu
kati ya 10 (32%) wa mijini walio na ujuzi huo wa msingi, kulinganisha na mtoto
1 tu kati ya 10 (11%) wa vijijini.
Utajiri Katika umri wa miaka 9,
ni watoto 2 tu kati ya 10 (21%) kutoka katika kaya tajiri zaidi walio na ujuzi
huo wa msingi, kulinganisha na chini ya mtoto 1 kati ya 10 (6%) kutoka kaya
maskini.
Aina ya Shule Katika umri wa miaka 9,
ni zaidi kidogo tu ya mtoto 1 kati ya 10 (15%) katika shule za umma aliyefaulu
majaribio hayo wakati ambapo ni watoto 4 kati ya 10 (39%) kutoka shule binafsi
walioweza kufanya hivyo.
“Kuna habari kuu mbili katika elimu ya
Tanzania leo,” alisema Zaida Mgalla, Mratibu wa Nchi wa Uwezo Tanzania “Kwanza, watoto walio wengi hawajifunzi kitu.
Pili, sisi ni jamii ya matabaka mawili – lile lenye utajiri zaidi au la mjini
au linaloweza kumudu gharama za shule za binafsi na hivyo watoto wao kufanya
vizuri zaidi shuleni kuliko watoto wengine.
Linapokuja suala la
elimu, Tanzania si nchi moja.” Tathmini ya Uwezo ya mwaka 2012 iliendeshwa na wananchi waliojitolea
7,560, ambao walisimamiwa na washirika katika wilaya 126 nchini (Wilaya za
Mtwara hazikujumuishwa kwa sababu viongozi wa Mkoa hawakuruhusu utafiti
kuendeshwa mwaka 2012). Lengo lilikuwa ni kuwashirikisha wananchi katika
mchakato wa kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuhakikisha watoto wetu
wanajifunza.
Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajani, alisema “Kuinua ubora wa elimu ni jukumu la msingi la
Serikali; hata hivyo jukumu hili inatuhusu sote. Hatua zichukuliwe katika ngazi
zote, na kila mmoja – kuanzia wazazi hadi watunga sera, kuanzia walimu hadi
maofisa wa wilaya – kila mmoja ana mchango wa kipekee katika kuhakikisha watoto
wetu wanajifunza.”
Mgeni Rasmi Salum Mjagila, Mkurugenzi, Elimu ya Watu Wazima MOEVT, akikabidhi ripoti kwa mwakilishi wa wanafunzi ambae pia ni ripota wa Uwezo TV, Bi. Fatma Bakari
Rakesh Rajani, John Ulanga, Zaida Mgalla na waalikwa wakifurahia jambo
No comments:
Post a Comment