Tangazo

January 17, 2014

TWANGA NA MSONDO KULA SAHANI MOJA CCM KATA 14 TEMEKE

Bendi za Muziki wa Dansi za African Stars "Twanga Pepeta" na Msondo Ngoma Music, Jumapili tarehe 19 Januari zimepanga kufanya onyesho moja kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.

Onyesho hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa C.C.M kata ya 14 wilayani Temeke na maandalizi yote yamekwisha malizika.

Bendi hizo ambazo zipo kwenye mahusiano mazuri ya muda mrefu, zimeamua kufanya onyesho hilo ili kuwapa burudani mashabiki wao kwa kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.

Kwa Upande wa Twanga Pepeta ambao kwa sasa wanatamba na albamu yao ya "Nyumbani ni Nyumbani" watatumia onyesho hilo ili kuwaonjesha mashabiki ladha mpya za 2014 wakiwa na wakali wao wote wakiongozwa na Kiongozi wao Luizer Mbutu.

Kwa Upande wa Msondo wao wanataraji kumualika aliyekuwa Kiongozi wao Mkuu Mzee Ngurumo ili aje kutoa sapoti ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.

Onyesho litaanza mapema saa 12 kwa Msondo kuanza kutoa burudani Kabla ya kuwaachia vijana wao kuendeleza kutoa burudani.

No comments: