Tangazo

March 27, 2014

SERIKALI YA UJERUMANI KUTUMIA EURO MILIONI 10 KUKARABATI RELI YA KATI

DSC_0001
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini, Dkt Frank-Walter Steinmeier wakiwasili kwenye chumba cha mkutano kuzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa MObog).

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania

SERIKALI ya Ujerumani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imeahidi kutumia zaidi ya Euro milioni 10 kukarabati reli ya kati (Central Line Railway). MOblog inaripoti.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini, Dkt Frank-Walter Steinmeier, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe amesema serikali ya Ujerumani imekubali kwa dhati kabisa kukarabati reli ya kati kwa manufaa ya Tanzania na nchi jirani.

“kwa sasa siwezi kusema ukarabati utaanza lini na jina la mwekezaji kwa sababu mazungumzo yanaendelea lakini kwa hakika kabisa tumeshakubaliana kwenye jambo la ukarabati wa reli ya kati,” amesema Waziri Membe

Amesema reli ya kati itapunguza matumizi ya barabara kwa mizigo na barabara za nchi zitakuwa salama na kuongeza tija katika Nyanja za biashara kupitia soko la pamoja Afrika Mashariki na kati.
DSC_0072
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Membe alilisisitiza kwamba ziara ya Waziri mpya wa mambo ya nje kutoka Ujerumani ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa sababu amekuja na wawekezaji 65 kutoka maeneo mbalimbali.

Amesema kuwa ukarabati wa reli ya kati ni muhimu katika kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili kwa maslahi ya watu wao.

“reli ya kati kama mnavyojua ilijengwa na Wajerumani mwaka 1913 na kwa sasa ina miaka karibu mia moja na kitu,” aliongeza Waziri Membe

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Steinmeier amesema kuwa nchi yake itaendelea kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na Tanzania katika jitihada za kuharakisha maendeleo ya nchi na watu wake.

Amesema kuwa serikali ya Ujerumani imeamua kukarabati reli ya kati katika jitihada za kukumbuka na kudumisha historia ya muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

“najisikia furaha na faraja kuona nchi yaTanzania inapiga hatua mbele kimaendeleo baada ya uhuru wake,” amesema
DSC_0096
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa kihistoria na kiuchumi kati ya Tanzania na Ujerumani jijini Dar es Salaam.
DSC_0112
Baadhi ya wageni waalikwa na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani nchini.
DSC_0043
Sehemu ya waandishi wa habari nchini pamoja na waandishi kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo leo jijini Dar.
DSC_0116
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
DSC_0122
Waziri Membe na mgeni wake wakiondoka kwenye chumba cha mkutano kuelekea Ikulu kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments: