1)Kuchunguza uendeshaji wa mkataba wa
kuzalisha Umeme kati ya kampuni ya IPTL na TANESCO
2)Kuchunguza kama wakati escrow
inafunguliwa kampuni ya mechmar ilikuwa inamiliki IPTL, kama ilikuwa imefilisiwa
na kama ilikuwa imehamisha umiliki wake kwa kampuni ya PAP.
3)Kuchunguza na kuthibitisha ushahidi
wa kampuni ya PAP kununua kampuni ya mechmar na kumiliki IPTL
4)Kuchunguza chanzo cha mgogoro kuhusu
tozo kati ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha ushahidi wowote kuwa mgogoro
uliamuliwa kwa faida ya IPTL
5)Kuchunguza kama ilikuwa sahihi kwa
mwanasheria mkuu wa Serikali kusamehe kodi ya VAT ya jumla ya tshs 26 bilioni
kutokana na tozo ya capacity charges na TRA wachukue hatua gani kuhakikisha
kodi hiyo inakusanywa
6)Kuchunguza kiwango cha fedha
kilichopaswa kuwemo katika akaunti ya escrow, kiwango gani kilikuwepo wakati
IPTL wanalipwa na kiwango gani kitapaswa kulipwa zaidi kutoka tanesco
7)Kuchunguza madai ya benki ya
standard chartered kwa tanesco na madai mengine yeyote yanayohusiana na mkataba
wa kuzalisha Umeme wa IPTL na iwapo Serikali imejihadhari na uwezekano wa madai
yanayoweza kufunguliwa, nafasi na heshima ya nchi katika kuheshimu mikataba ya
kimataifa na ya uwekezaji.
8)Kuchunguza iwapo Wizara ya Nishati
na madini ambayo ni mhusika Mkuu wa akaunti ya tegeta escrow ilifanya 'due
diligence' ya kutosha kabla ya kuingia makubaliano ya kutoa fedha zilizopo
akaunti ya tegeta escrow. Kupata Maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
madini ni kwa nini aliagiza ukaguzi maalum wakati yeye ni mhusika Mkuu kwenye
mchakato mzima na ilhali akijua PAC tayari imeanza mchakato wa ukaguzi.
9)Kutoa mapendekezo ya njia bora za
kisheria kulinda Taifa kutoingia hasara zaidi katika mkataba wa IPTL chini ya
wamiliki wapya
10)Kutoa ushauri kwa kamati ya PAC juu
ya mapendekezo ya hatua ambazo Bunge linapaswa kuchukua kuhusu matokeo ya
ukaguzi huu maalumu
No comments:
Post a Comment