Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe inayowawezesha
wateja wake kununua simu ya kisasa ya aina Samsung S5 na kupata
vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.
Akiongea
wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde
alisema” leo tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo
inawawezesha kununua simu ya Samsung S5 na kupata dakika 1500 bure , SMS
5000 kutuma mitandao yote pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB
kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi katika mitandao kama vile
facebook na twitter kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G yenye kasi
zaidi.
Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya Samsaung S5”.
Simu
hii ya Samsung S5 inapatikana katika maduka ya Airtel yaliyopo Moroco,
Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka yote ya Samsung pamoja na maduka
yanayouza simu za smart phones yaliyoko nchi nzima.
Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde
No comments:
Post a Comment