Tangazo

April 11, 2014

DAKIKA 20 ZILIZOMPA MASWALI NA MAJIBU KINANA ALIPOTEMBELEA MAPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

  • Asimama kwa dakika 20 kuangalia shughuli za kila siku mpakani mwa Tanzania na Burundi, ajiuliza maswali mengi na kupata majibu, atoa ushauri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
  • Ajionea maisha halisi ya watu wa mpakani mwa Tanzania na Burundi
  • Ashindwa kuelewa kwa nini soko la mifugo lilikufa
  • Ashangaa viongozi kutokuwa wabunifu hasa katika fursa zinazoweza kuwasaidia wananchi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama mpakani mwa Tanzania na Burundi katika kijiji cha Kibande wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma akiangalia upande wa Burundi kwenye kijiji cha Murambi.
 Watu wakivuka Mto Malagarasi wakitokea Burundi ambako huuza na kununua bidhaa zao kwenye soko la mchana maarufu kama soko la Buhija.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma kuelekea kwenye mkutano wa hadhara baada ya kushuhudia mfumo mzima wa maisha ya mpakani mwa Tanzania na Burundi.
 Hili ndio soko la mchana la Buhija ambapo Watanzania wengi wanaoishi wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma hufanya shughuli zao za biashara, soko hili lipo nchini Burundi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikata muwa ambao aliununua kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa mpakani mwa Tanzania na Burundi

No comments: