Tangazo

April 8, 2014

MBUNGE WA KIGAMBONI ATEMBELEA KITUO CHA AFYA KIGAMBONI KUANGALIA MAENDELEO YA TIBA YA KANSA YA KIZAZI KWA KINAMAMA

 Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (mwenye fulana ya mistari mbele) akizungumza na baadhi ya kinamama wakazi wa Mji wa Kigamboni waliojitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi kwa kina mama inayoendelea kutolewa kituoni hapo.
  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akimuuliza Muuguzi wa zamu namna zoezi hilo la Utoaji wa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye Kituo cha Afya Kigamboni.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kigamboni,Dkt. Ansilla Lasway (kushoto) akimueleza Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile namna wanavyoendelea kutoa huduma za matibabu mbali mbali kwa wananchi wa Kigamboni.Mh. Ndugulile alitembelea kituo hicho leo ili kuona namna huduma zinavyotolewa kwa wagonjwa na changamoto zinazokikabili kituo hicho na kuahidi kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
 Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile akiwapongeza kinamama wa Kigamboni kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Kituo cha Afya Kigamboni na kwa ajili ya kupatiwa Huduma ya Uchunguzi na Tiba ya Kansa ya Mlango wa Kizazi inavyoendelea kwenye kituo hicho.

No comments: