Tangazo

April 5, 2014

RIDHIWANI AITEKA PERA

 Mke wa Ridhiwani Kikwete ,Arafa akimuombea kura mumewe kwa wananchi wa kata ya Pera
 Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 Ridhiwani Kikwete akihutbia wakazi wa kata ya Pera kwenye mkutano mkubwa wa hadhara  uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Pera shuleni na kuwahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze kuwa atakuwa Mbunge wa Vitendo zaidi na kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya Jimbo.
 Wananchi wa Kata ya Pera wakimsikiliza mgombea wa ubunge wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
 :
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Mwigulu Nchema akihutubia wakazi wa Pera na kuwaambia wapinzani wao wanajua kubisha hata kwenye jambo lisilohitaji ubishi hivyo kusababisha kupoteza muda wa kujadili masuala ya msingi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Pera na kuwaambia mwisho wa wapinzani Chalinze ni tarehe 6 siku ya kupiga kura.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge akihutubia wakazi wa Pera ,Chalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Pera Shuleni.
 Kila mwenye uwezo wa kucheza alicheza.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda akicheza na Vijana wa CCM linalofahamika kama Tanga All Stars.

No comments: