Tangazo

May 15, 2014

MISS DAR CITY CENTRE 2014 TALENT SHOW KUTIKISA MAISHA CLUB



 Warembo wanaowania taji la Miss Dar City Center 2014 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa Habari hii leo.
Mratibu wa shindano hilo, Judith Michael akizungumza na wanahabari, pamoja nae ni Mkufunzi wa warembo hao. 
 *********
Na Father Kidevu Blog 
WANYANGE 20 wanao wania taji la Miss Dar City Center kesho Mei 16 mwaka huu watawasha moto vikali katika ukumbi wa Maisha Clab wakati wa shindano lao la Vipaji.

Shindano hilo litaongozwa na wasanii, Rich Mavoko, Bonge la Nyau na TID ‘Mnyama’ wanataraji kuwaongoza warembo hao kuwania taji la Vipaji 'Miss Talent Dar City Center 2014."

Akizunguumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo mratibu wa Shindano hilo, Judith Michael Amesema warembo wote 20 wapo katika hali nzuri na wamejifua vya kutosha kwaajili ya shindano hilo la vipaji.

“Tunaamini shindano la mwaka huu litakuwa zuri sana warembo wamejiandaa vya kutosha, tunapenda kwaalika wadau mbalimbali wa masuala ya urembo waje kwa wingi Club Maisha siku hiyo ya Ijumaa ili waweze kushuhudia wenyewe jinsi warembo wa jiji letu walivyojaliwa vijapaji hakika miss Tanzania yupo Dar City Centre,” alisema Judith.

Aidha Judith amesema shindano la Miss Dar City Centre litafanyika Mei 24 mwaka huu katika ukumbi wa Escape One Mikocheni ambapo pia ameahidi shindano hilo kuwa la aina yake.

Judith amewataja warembo wanao wania taji hilo kuwa ni pamoja na Naomy Kisaka,  Nasreen Abdul, Gladys Matson, Habiba Israel, Jenny Zahn,
Doreen Elias, Winniefrida   Msusa, Grace Mella na Rehema Athumani.

Wanyange wengine ni Francisca Simon, Salha Suleiman, Dorica Daud, Agriphina Yelezwa, Sabina Thomas, Jihan Dimachk, Aziza Thabiti, Hatma Rshidi Nyembo na Neema Sisamo.

Huku wadhamini wa Shindano hilo la Miss Dar City Centre ni Prima Total Hair Collection,Gumbo Investment Diamond Bureau Dechange, Father Kidevu Blog, Maisha Club,Q Plus, Zanzi Cream, Clouds Fm, Machapta, Flamour Cosmetics, Valley Spring, Best Point Hotel, Atik Aluminium, Jambo Leo, Blog Ya Wananchi na Skylight Band.

No comments: