Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais
wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Mama Asha Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya
Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika jana
Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe, Malawi. Picha na
OMR
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Lilongwe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, leo Jumapili Julai 06, 2014 ameiwakilisha Tanzania
katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Malawi, sherehe zilizofanyika
katika Uwanja wa Civo jijini Lilongwe.
Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania,
pia alihudhuria Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Waziri Mkuu wa Msumbiji na
viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika.
Sherehe hizo zilianza kwa ibada ya misa asubuhi na kisha
kuhamia katika uwanja wa Civo mchana ambapo Rais wa Malawi Prof. Athur
Peter Mutharika alikagua gwaride na kisha kuwasha Mwenye wa Jubilee ya miaka
50 na baadaye kulihutubia taifa.
Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Mutharika alisisitiza
kuhusu umuhimu wananchi wa Malawi kuwa wamoja na akaeleza nia yake ya
kujenga umoja kwa nchi zinazoizunguka Malawi pamoja na zile za Kusini mwa
Afrika. Baada ya hotuba hiyo, sherehe hizo ziliendelea na mchezo wa soka
baina ya timu ya taifa ya Malawi na Msumbiji.
Malawi ilipata uhuru wake mwaka 1984 ikiongozwa na Rais wake
wa kwanza Dkt. Kamuzu Banda hadi mwaka 1994. Baada ya mwaka huo alifuata Rais
Dkt. Bakili Muluzi aliyetawala kuanzia mwaka 1994 hadi 2004.
Baaada ya mwaka huo alifuata Rais Profesa Bingu wa Mutharika
aliyetawala hadi mauti yalipomkuta mwaka 2012. Dkt. Joyce Banda aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Mutharika alichukua madaraka na kukaa hadi mwaka huu 2014
ambapo Malawi iliingia katika uchaguzi mkuu na kisha Rais Profesa Arthur Peter
Mutharika aliposhinda uchaguzi huo na hivyo kuwa Rais wa nne wa Malawi.
Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana
na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi
Juma Maalim na Mheshimiwa Makamu wa Rais amerejea nyumbani Tanzania Julai 07,
2014 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai 06, 2014 Lilongwe: Malawi
|
No comments:
Post a Comment