Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni,Joseph
Nicholous 9kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,
ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba mfano
wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 ikiwa ni msaada uliotolewa na TBL
kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar
es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati hiyo.
Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya
Makuburi.James Ngoitanile.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba (wa pili kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 Mkurugenzi wa Kampuni ya Drima Drilling, Mhandisi Amiri Msangi msaada uliotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati hiyo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya Makuburi.James Ngoitanile.
Jengo la zahanati ya Makuburi
Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni,viongozi wa na wahudumu wa zahanati hiyo pamoja na Wajumbe wa kamati ya maji ya mtaa huo Mwongozo wakifurahia kupata msaada huo kutoka TBL.
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya kampuni hiyo kutoa sehemu ya faida ya mauzo ya vinywaji vyao kuwapatia wananchi misaada ya maji nchini.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Kamaba akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo wa kisima cha maji.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Kivugo akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada wa kisima cha maji na kwamba kitendo hicho kitawapunguzia kwa asilimia kuwa tatizo la maji lililokuwa linaikumba zahanati hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkazi wa Makuburi, akielezea kwa hisia kufurahishwa na msaada huo wa TBL kwa wakazi wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment