Tangazo

July 3, 2014

Mazishi ya Mwanahabari Nguli nchini, Mzee Nkwabi Ng’wanakilala

Mhariri wa gazeti la ThisDay, Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo  (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwaajili mazishi. Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI
Mzee Nkwabi Ng'wanakilala enzi za uhai wake.
Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa wenye sura za majonzi baada ya kuuga mwili wa Marehemu. Kutoka (kushoto), Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara ya Katiba na Sheria, Omega Ngole, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Raphael Hokororo na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Raia Mwema, Godfrey Dilunga.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Marehemu Mwl. Ng’wanakilala.
Mjane wa Marehemu, Nadhira Ng’wanakilala akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mume wake  Marehemu Mwl. Ng’wanakilala.
Watoto wa kike wa Marehemu wakitia udongo ndani ya kaburi la mpendwa baba yao wakati wa mazishi.
Mtoto mkubwa wa marehemu, Lulu Nkwabi Ng’wanakilala akiweka shada la maua kwa niaba ya watoto wa kike.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangaji Tanzania (TBC), Clement Mshana akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Marehemu Mwl. Ng’wanakilala.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Marehemu Mwl. Ng’wanakilala.
Wanahabari wakongwe nchini (kutoka kushoto), Evarist Mwitumba, Lucas Liganga na Bob Karashani nao walikuwa miongoni mwa waombolezaji.

No comments: