Tangazo

October 4, 2014

KIPINDI CHA "MIMI NA TANZANIA" CHAWASHUKURU WATANZANIA KWA KUCHANGIA MATIBABU

10311052_1940774076061511_5395068416549286320_n
Pichani ni Zuhura Matata mgonjwa mwenye uhitaji wa upasuaji utakaofanyika nchini India.

Kipindi cha “Mimi na Tanzania” kinachoongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu, kinatoa shukrani kwa watanzania wote walioguswa na kufanikisha michango ya matibabu ya Zuhura Matata mwenye tatizo la kuvimba mguu ambao unahitaji Oparesheni nchini India.

Kupitia Akaunti yake ya mtandao wa kijamii Facebook muongozaji wa kipindi hicho Hoyce Temu ameandikia ujumbe wa kuwashukuru watanzania. Soma hapa chini.
Untitled
Zuhura Matata ambaye tulimuombea msaada wa kwenda India kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania, amefanikiwa kupata pesa zote shilingi milioni 15 sawa na dola elfu kumi. Ataondoka tarehe 21 Oktoba kuelekea India na kuanza Matibabu! Usikose kutazama kipindi cha Mimi na Tanzania, Jumapili, Chanel Ten kuanzia saa tatu na nusu usiku. Mimi Hoyce Temu natangaza rasmi kufunga michango kuanzia sasa kwani pesa tulizoomba tumepata zote! Asanteni Tanzania!
10639696_1940773056061613_8215664022486093041_n
Pichani ni Mtangazaji wa Kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu alipomtembelea Zuhura Matata kwa ajili ya mahojiano.

No comments: