Tangazo

October 1, 2014

MATUKIO MBALI MABLI YA SHUGULI ZA WAZIRI MKUU PINDA DODOMA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kwenye viwanja vya Bunge  mjini Dodoma Oktoba 1, 2014. Kutoka kushoto ni  Sophia Simba, Kingunge Ngombale- Mwiru na John Shibuda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba wakifurahia jambo katika mazungumzo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Oktoba 1, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) wakizungumza na viongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Room to Read , Ofisa Mkuu (Chief Program Officer), Cory Heyman  (wapili kulia) na Mkurugenzi mwendeshaji ( Program Operations Officer), Stephen Chimalo, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma, October 1, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma October 1, 2014. Kutoka kushoto ni Emmanuel Nchimbi, Ridhiwani Kikwete na Dr. Asha-Rose Migiro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Kazi cha Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua kikao hicho mjini  Dodoma October 1, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kulia), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia (wapili kulia) na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba baada ya kufungua kikao cha kazi cha viongozi wa mikoa, wilaya na Halmashauri mjini Dodoma Oktoba 1, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: