Kile
kinachoonekana kama aina fulani ya urasimu, upasuaji (postmortem) wa
mwili wa dansa Aisha Madinda uliokuwa ufanyike leo mchana (Alhamisi)
umeshindikana na sasa utafanyika kesho (Ijumaa) asubuhi.
Meneja
wa Aset, Hassan Rehani ameiambia Saluti5 kuwa mwili wa Aisha
aliyefariki Jumatano asubuhi ulihamishwa kutoka Mwananyamala Hospitali
kwenda Muhimbili kwaajili ya upasuaji ili kujua chanzo cha kifo, lakini
ikashindikana kwa madai ya muda wa kufanya upasuaji umekwisha.
Hassan
Rehani amesema Muhimbili wamedai mwisho wa kufanya ‘postmortem’
unakwisha saa nne asubuhi na hivyo zoezi hilo sasa litafanyika Ijumaa
asubuhi chini ya usimamizi wa polisi.
Kwa
hali ilivyo, kama utatokea urasimu au ucheleweshaji wowote wa kuufanyia
uchunguzi wa mwili wa Aisha Madinda, basi ni wazi kuwa ratiba ya
mazishi inaweza kubadilika.
Aisha
Madinda alitarajiwa kuzikwa Kigamboni Ijumaa mchana mara baada ya sala
ya Ijumaa. Mwanzoni kabila ilikuwa azikwe Alhamisi saa 10.
Wakati
familia ya Aisha Madinda ilikuwa radhi kumzika ndugu yao bila ya
uchunguzi zaidi, polisi iligoma kabisa na kusema kwa mazingira ya kifo
chake, upasuaji ni suala la lazima. Source Saluti5
No comments:
Post a Comment