Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya King’ongo wakifurahia vitabu vya
masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Airtel Shule Yetu’ kukabidhi vitabu vyenye
thamani ya milioni 4/- kwa shule hiyo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara
jijini Dar es Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu
ya mkononi ya Airtel imetoa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Shule ya
Sekondari ya King’ongo iliyopo Kimara katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam.
Vitabu hivyo
vyenye thamani ya shilingi million 4 vilitolewa na Airtel chini ya mradi wa
Airtel shule yetu lengo likiwa nikusaidia kutatua uhaba wa vitabu mashuleni na
kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za sekondari nchini.
Akiongea wakati
wa halfla ya kukabithi vitabu Meneja huduma kwa jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi
alisema “Tangu mradi uanze takribani miaka 10 iliyopita tumeweza kuzifikia
shule nyingi hususani shule zenye uwiano wa wasichana wengi zaidi. Tunaamini
mradi huu utaendelea kuwawezesha wanafunzi wengi kupata nyenzo za masomo
nakuwapatia motisha wasichana kujiunga na masomo ya sayansi na kuwaendeleza
zaidi kielimu kwani tunatambua tukimuwezesha mwanamke tumewawezesha jamii kwa
ujumla.
Tunatoa wito
kwa wanafunzi kuvitumia na kuvitunza vitabu hivi vizuri ili viweze kutoa tija
kwa wanafunzi waliopo na watakao jiunga na shule hii, tunaahidi kuendelea
kuziwezesha shule nyingi zaidi kupata vifaa muhimu vya masomo kwa njia za
kielectronikia kwa nji ya mtandao mkakati utakaotambulishwa hivi karibuni.
Aidha Airtel
kupitia wafanyakazi chini ya mpango wake wa Airtel tunakujali bado pia
wanaendelea na mkakati wakusaidia maendeleo ya shule mbalimbali nchini. Chini
yamradi wake wa Airtel Tunakujali shule mbalimbali ikiwemo shule ya ushindi
jijini Dar esa saalam zimefaidika kwa kufanyiwa ukarabati wa darasa la awali
shule.
Sambamba na hilo shule ya watoto wenye mahitaji maalumu ya pongwe
mkoani tanga nayo imepata msaada wa kujengewa darasa ambalo linategemea
kukabithiwa rasmi mwisho mwa mwezi huu kupitia Airtel Tunakujali.
Miradi hii yote
ya Airtel Shule yetu na Airtel Tunakujali inalengo la kuziwezesha jamii
zinazotuzunguka kuwa na mazingira bora yatakayowezesha utoaji wa elimu bora kwa
watanzania na jamii kwa ujumla.Aliongeza Bayumi.
Kwa upande wake
Mkuu wa shule ya sekondari ya King’ongo Nyaibuli Bhoke alisema “ tunawashukuru
sana Airtel kwa kuleta msaada huu wa vitabu shuleni hapa, shule yetu imekuwa na
upungufu wa vitabu hivyo msaada huu umekuja kwa wakati muafaka. Natoa wito kwa
wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivi kwa kuvisoma ili viweze kuongeza ufaulu
shuleni hapa.
No comments:
Post a Comment