Akizungumza
na blog hii Mkuu wa wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa awataka wananchi wa wilaya
hiyo kusoma na kuijadili katiba hiyo na kutosikiliza kutoka kwa watu.
Aidha
Mtasiwa amesisitiza kuwa Tanzania bado tunakatiba yetu na tupo kwenye mchakato
wa kupata katiba mpya hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na maneno wanayo
ambiwa na watu wengine.
“Katiba
inayopendekezwa imeandikwa na binadamu wa kawaida kama ilivyokuwa hapo awari
katika katiba ambayo inatumika hadi sasa lakini inapaswa kuangalia kuna mambo
gani mapya ambayo yameandikwa kwenye katiba inayopendekezwa na imebeba mambo
gani muhimu katika maendeleo ya Tanzania yetu”.alisema mtasiwa
Lakini
Mtasiwa ameendelea kuwataka watanzania kwa ujumla kuendelea kuidhamini amani
tulivyo nayo kwa sasa na tusiwafuate wananchi wengi wenye lengo la kuvuruga
amani yetu kwa maslai yao binafsi hivyo watanzania msidaganyike kwa maneno yao.
Mtasiwa amewaomba
wazazi wote kuwapa elimu ya kutosha watoto wao juu ya kutunza amani na kuacha
tabia ya kushabikia maneno ya uchochezi yenye lengo la kuvuga amani yetu.
Wakati
huohuo Mtasiwa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujua umuhimu wa kutumia bima
na wajitokeze kuchangia katika mifuko ya bima.
Bima ya afya
inafaida kubwa sana katika maisha yako hivyo lazima wananchi watambue umuhimu
wa kuchangia bima kwa kuwa serikali imepanga kuwachangia wananchi kwa kiasi
kile ambacho wamekichanga kwa mfano wananchi wakichanga milioni 100 na serikali
itatoa milioni 100 kwa lengo la kuboresha sekta ya afya.alisema Mtasiwa.
1 comment:
thanks for sharing good information
Post a Comment