Meneja Masoko wa
Airtel, Aneth Muga akionyesha kwa wanahabari (hawapo pichani) simu ya kisasa ya
Airtel Red itakayopatikana kwa gharama nafuu katika Airtel Bazaar.
|
Meneja
Masoko wa Huawei, Lydia Wangari akionyesha kati ya simu mbili zitakazouzwa na
ofa ya 'Pata Moja BURE'
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
* Ofa kabambe ya simu za Smart phone kutoka Huawei zikiwa
zimeunganishwa na Airtel
* Simu kuuzwa bei poa zikiwa na ofa za vifurushi kabambe kutoka Airtel
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ikishiriakiana na Huawei leo imetangaza kuanza Bazaar lake maalum litakalowawezeha watanzania kujipatia simu za kisasa za Smart phone na kuweza kufurahia huduma za zote za intaneti kupitia mtandao wa Airtel.
Bazaar la Airtel na Huawei limepangwa kufanyika kuanzia ijumaa, jumamosi
na jumapili hii kuanzia saa 3asubuhu hadi saa moja usiku katika eneo la ndani
la Mlimani City na litakuwa na muendelezo hapo hapo na baadae litazunguka
katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumzia Bazaar hilo Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema "Bazaar
letu litakuwa la kijanja zaidi kwani simu za smart phone zitakazouzwa ni bora
na zitaambatana na ofa kabambe kuliko zote zinazopatikana sehemu yoyote".
"Mteja wetu uliopo mahali popote tembelea BAZAAR la Airtel ujinyakulie simu
bora na kisasa kama zile za Huawei au Airtel Red kwa punguzo kabambe zikiwa
na kifurushi cha intaneti kitakachokupa MB 120, SMS 120 pamoja na muda wa
maongezi 120 ofa ambapo huwezi kuipata popote zaidi ya kweye Airtel
Bazaar" alisema Muga.
Meneja masoko kutoka Huawei Lyidia Wangari aliongeza kuwa licha ya simu za
Smart phone za Huawei kuuzwa kwa gharama nafuu pia atakaenunua simu pale
atajipatia simu nyingine ya bure au zawadi tofauti tofauti papo hapo kwa mfano
"mteja yeyote kati ya 300 wa kwanza kununua simu ya Huawei aina ya Met 7
DUAL atapata simu aina ya Kishkwambi bure kabisa na atakaenunua simu ya Huawei
Met 7 atapata simu ya bure aina ya Y220 pale pale" alifafanua
Kwa Upande wake Afisa Airte l wa kitengo cha Smartphone Bw, James Kagashe
alisema "tunataka kudhihirisha kwa wateja wetu kuwa Airtel ndio mtandao
sahihi kwa Smartphone yako popote ulipo, nakuhakikishia kuwa kila simu
inayouzwa katika Artel Bazaar inakuja na ofa kabambe ya kifurushi cha SMS,
dakika za muda wa maongezi pamoja na intanet itakayokuwezesha kuperuzi
upendavyo"
Nawahamasisha wale wote mnaotaka kuenda na wakati kwa kumiliki simu bora na
kuunganishwa na mtandao bora kwa Smartphone yako tembelea Airtel Bazaar la
Airtel Mlimani City ili tukuunganishe. Alimaliza kwa kusema Bw Mwanda.
No comments:
Post a Comment