Mhandisi mashuhuri
George Mulamula (pichani), ameipongeza programu mpya ya Airtel Tanzania
ijulikanayo kama “Airtel Fursa” inayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo
kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli
zao.
Kama mmoja wa jopo la
washauri ambaye atachagua vijana watakaotimiza vigezo vya kuweza kuingia
katika mpango wa Airtel Fursa.
"Hii ni nafasi
nzuri ya kuleta mabadiliko, kuhamasisha vijana na kuwasaidia kujijenga
kibiashara endelevu na ninapenda kuwapongeza Airtel kwa ajili ya mpango
huu," alisema Mulamula.
Bwana Mulamula aliahidi
kufanya kazi kwa karibu na Airtel pamoja na jopo la washauri katika
kuhakikisha wanachagua na kuwapa mafunzo walengwa wa Airtel Fursa ikiwa
ni pamoja na kuwasaidia kuweza kutumia techonologia ya habari yaani ICT kama
nyenzo muhimu itakayowawezesha kuleta ufanisi katika shughuli zao za
uzalishaji na kiuchumi. Akiamini kuwa vijana watakaofaidiaka na Airtel
fulsa watahamasisha na kuongoza katika kuleta mabadiiko kwenye jamii zao huku
akihakikisha mpango huu unakuwa na mafanikio makubwa kwa walengwa na kuwa
na mvuto kwa vijana wengine .
Mhandisi Mulamula ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama (ICT) Business Incubator (DTBi) kwa
ajili ya ujasiriamali katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), analeta
uzoefu wa kutosha katika mpango huu wa Airtel fursa kwenye nyanja ya
ujasiriamali na kukuza biashara zinazoanza.
Yeye ni mshauri na
mwalimu kwa wajasiriamali. Amekuwa akisaidia kuinua vipaji vya watu mbalimbali
hapa nchini na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na katika mkutano wa kimataifa wa
ujasiriamali nchini Moscow, Durban na Nairobi kwa ajili ya maonyesho ya Afrika.
Pia ni Mjumbe wa Bodi ya Demeter nchini Boston USA na pia Mjumbe wa Bodi ya
XPrize nje ya California, Marekani.
“Mpango huu unatafuta vijana wenye kiu,
nguvu na utayari wakupata wanachokiamini na kukihitaji, wenye uwezo wa
kuzipitia changamoto na kufikia matarajio waliojiwekea na wakati huohuo
kubadilisha maisha yao” aliongeza
Airtel Fursa inawalenga vijana wenye umri
kati ya miaka 18-24 ambao ni watanzania waishio nchini Tanzania. Vijana hao ni
lazima wawe wamiliki wa biashara ndogondogo, wenye hali ya ushindani na
kuheshimu biashara zao. Maelfu ya vijana watapata mafunzo kupitia warsha
mbalimbali na kupatiwa vitendea kazi vitakavyo boresha biashara zao.
Hii inajumuisha mafunzo katika usimamizi
wa fedha, mikopo, faida za kuwa na akaunti ya benki na usimamizi wa biashara
kwa ujumla
Wanaotaka kujiunga wanapaswa kutuma
ujumbe mfupi kwenda 15626 ukiambatanishwa na taarifa zifuatazo;- jina,
umri,aina ya biashara, mahali na namba ya simu. Airtel Fursa pia inakaribisha
mapendekezo ya vijana wenye vigezo husika.
Maombi yanaweza kutumwa pia kwa njia ya
barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com
au tovuti ya Airtel. Maombi yaambatanishwe na jina, umri, aina ya biashara,
mahali, namba ya simu na sababu ya kusaidiwa kibiashara.
No comments:
Post a Comment