Wafanyakazi wa Airtel wakiwa
katika picha ya pamoja na Bertha Benedict (wapili Kulia) mara baada ya
kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kutoka kushoto ni
Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, mama yake
Bertha, Hawa Bayumi na Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kusini , Fadhili
Mwasijeba.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Kampuni
ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambao
umelenga kuwawezesha vijana wajasiliamali wadogo wadogo nchini umetoa msaada
mwingine tena jijini Dar es salaam kwa msichana mjasiriamali Bertha Benedicto.
Bertha
ambaye amelelewa katika Kituo cha Kulea watoto cha Dogodogo Center Kilichopo
Bunju Jijini Dar es Salaam na kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja ya ufundi wa
kushona nguo kituoni hapo amepatiwa vifaa mbalimbali pamoja na cherehani ya
kisasa ili kuendeleza ujuzi wake.
Akiongea
wakati wa makabithiano Meneja wa mahusiano ya jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi
alisema “ Airtel tumeona ni vyema kupitia mpango wetu wa Airtel Fursa
kumpatia vifaa na mashine hii ya kisasa ya kushonea Bi Bertha Benedecto
kwa lengo la kumwezesha kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi
zaidi.
Sambamba na hilo tumeweza kumpeleka kwenye mafunzo ya
kumsaidia kujijenga, kuweka mahesabu yake na kuendesha biashara yake ili
aweze kukuza biashara na kuisaidia familia yake”.
Tunaamini
hii ni nafasi ya pekee kwa vijana wadogo kati ya umri wa miaka 17 mpaka 24
walioko katika maeneo mbalimbali ya nchi kuweza kufaidika na mpango huu wa
Airtel Fursa wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali wadogo wadogo
kukuza mitaji na biashara zao kwa ujumla". Aliongeza Bayumi
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo, Bertha amesema vifaa hivyo vitamwezesha
kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla huku Mama yake Immaculate Makinda
akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.
Bertha
alisema, “nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu. Kwa
kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa. Nimekuwa nikipata ugumu wa kupata
wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji
ya wateja wangu lakini sasa naamini nitapata wateja wengi sana na kuinua
biashara yangu”
Kwa
upande wake Mratibu wa Dogodogo Centre, bw.Issa Buzohela alisema, anaiomba
kampuni ya Simu ya Airtel kuendelea kukisaidia kituo hicho na kuinua
vipaji vya vijana kwani nchi yetu imezungukwa na vijana wenye vipaji mbalimbali
lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.
Mpaka
sasa Airtel Fursa imeshawawezesha vijana mbalimbali na kuboresha shughuli
zao za kiuchumi kwa kuwapatia vitendea kazi na kuwaingiza katika warsha
za mfunzo ya Airtel Fursa ili waweze kutimiza ndoto zao.
No comments:
Post a Comment