Tangazo

June 24, 2015

ZIARA YA KINANA MISUNGWI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Misungwi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Amani ikiwa muendelezo wa ziara za kukagua,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Umati wa wakazi wa Misungwi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia kwenye uwanja wa Amani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Misungwi ambapo aliwaambia hakuna namna CCM itaibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu tarehe 25, Oktoba mwaka huu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Misungwi mkoani Mwanza.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi akitoa salaam za ukaribisho kwa ugeni wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Mbunge wa Jimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulika na Madini Mhe. Charles Kitwanga akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Amani na kueleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM unavyoenda vizuri.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo akiwasalimu wakazi wa Misungwi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Amani kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara mkoani Mwanza yenye malengo ya kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Amani, Misungwi ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mbunge wa Jimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri Madini Mhe. Charles Kitwanga (kushoto) wakifurahia jambo pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (katikati) na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Amani,Misungwi mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akishirikia parizi katika shamba la dengu lililopo Misasi wilayani Misungwi, wengine wanaoshiriki pamoja na Katibu Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo (kushoto) na Afisa Kilimo kata ya Misasi Bi.Teresia Mathew Mkindo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Afisa Kilimo wa kata ya Misasi Bi. Teresia Mathew Mkindo mara baada ya kushiriki parizi , Misungwi mkoani Mwanza.
 Wasanii wa kikundi cha upendo wakipiga ngoma ya Kisukuma kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kata yao ya Misasi wilayani Misungwi.


 Wananchi wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Misasi, Misungwi mkoani Mwanza.
Wananchi wa kata ya Misasi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi Bi. Salome Samuel kadi ya uanachama wa CCM ,zaidi ya watu 300 wamejiunga na CCM katika kata ya Misasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na wananchi wa kata ya Mahando waliojitokeza kumpokea.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Misungwi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe.Charles Kitwanga wakisalimiana na wananchi wa Mahando.
Vijana wa Stendi ya Misungwi wakionyesha bango lenye ujumbe wa kukubali kazi ya Mbunge wao wakati wa ujio wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na mamalishe wa soko kuu la  Misungwi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisomewa risala na Mama Lishe wa Misungwi ambao walimueleza mambo matatu ya msingi kwao ambayo ni Mtaji mdogo,Sehemu hadimu za kufanya shughuli zao hivyo kuomba kujengewa na mwisho waliomba kuwe na taa usiku kucha kwenye stendi ya basi iwasaidie kuuza chakula na usiku.
(Picha zote na Adam Mzee)

No comments: