Meneja Huduma
kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akikabidhi hundi yenye dhamani ya
sh.milioni 20 ya msaada wa vyakula kwa BAKWATA kwa vituo mbalimbali vya watoto
yatima hapa nchini, akipokea (Kulia) Sheikh Mohamed Khamis Said mwakilishi wa
Bakwata.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na
Mwandishi wetu
Airtel
Tanzania imetoa Tsh Milioni 20 kwa Jumuiya ya Waislamu kupitia Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kufuturisha vituo kumi vya
kulelea watoto yatima nchini.
Akikabidhi
hundi kwa Naibu katibu Mkuu wa Bakwata Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Hawa
Bayumi alisema vituo vitakavyopata msaada huo ni pamoja na Kigogo Fresh
orphanage cha Ilala, IHSANI orphanage cha Temeke, Almadina center
kinondoni.pia kwa Arusha ni Kiboa Islamic orphanage, Nusuru yatima orphanage
Bukoba, Nuru orphanage Mbeya, Zam zam orphanage Dodoma, Maua Daftari
Foundation Zanzibar, Chuno orphanage
center Mtwara na Makorora Yatima
center cha Tanga ambapo kila kimoja kitapatiwa vyakula vyenye thamani ya
shilingi milioni2.
“Airtel
Tanzania kama inavyofanya miaka mingine leo pia inaungana na ndugu na jamaa
zetu waislamu kuadhimisha mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa kuwakumbuka watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia hivi vituo ili nao waweze
kushiriki mfungo wa Ramadhan.” alisema.
Aliongeza
kuwa Airtel imekuwa ikitoa misaada kama hii kwa makundi mbalimbali katika jamii
kila mwaka na kusisitiza kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Airtel watajumuika na watoto
hawa katika mwezi huu ili na wao pia wajiskie kama sehemu ya jamii.
“Tunapenda
kutoa rai kwa mashirika mengine pia yawakumbuke hawa watoto na kuwasaidia ili
wajisikie kama sehemu ya jamii,” alisema.
Akipokea
hundi hiyo, Naibu katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mohamed Khamis Said
aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo na kusisitiza kuwa utasaidia kwa
kiasi kikubwa na kuhakikisha watoto wanaolelewa katika vituo hivi wanapata
mahitaji muhimu hasa katika mwezi huu wa Ramadhan.
“Tunashukuru
mno kwa niaba ya vituo hivi na tunatoa wito kwa mashirika mengine pia
yajitokeze na kutuunga mkono ili tuweze kufikia yatima wengi zaidi na kuwapa
faraja katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan” alisema.
No comments:
Post a Comment