Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana. |
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha
na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO),
Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia
mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini
Mtwara jana.
XXXXXXXXXXXXXXXX
MTWARA
Vijana mkoani Mtwara
wametakiwa kutumia fursa za uwepo wa nishati ya mafuta na gesi katika kukuza
biashara zao na uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza mara baada ya
kumalizika kwa mafunzo ya ujasiriamali mkoani humo, baadhi ya vijana hao
wamesema kuwa fursa zilzizopo mkoani humo ni lazima ziwanufaishe vijana ili
waendane na ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.
Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mradi wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo na kuwawezesha mitaji baadhi ya vijana wa manispaa ya mtwara kwa lengo la kuwawezesha kumudu uendeshaji biashara zao na kukuza mitaji yao.
Idd Abdallah ni mjasiriamali
aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye anasema kuwa kwa sasa amepata muongozo
mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi.
“Hii ni fursa ya kipekee
kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu
na vijana wenzangu wa hapa mtwara” Alisema Abdallah.
Nae mkuu wa wilaya ya Mtwara bi.Fatuma Ally, alisema “mafunzo haya yatapanua wigo wa ufahamu kwa vijana hawa ambapo aliwataka kujituma kwani fursa zipo nyingi mkoani humo.
“Mtwara kuna maeneo mengi
sana yenye fursa kwa vijana kujiendeleza hivyo nawataka vijana kutumia fursa na
mafunzo haya kuhakikisha wanajiendeleza kiuchumi” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Hawa Bayumi ni Meneja Maendeleo ya Jamii wa Airtel, alisema hiyo ni fursa inatolewa na
Airtel kwa lengo la kusaidia vijana kupata fursa ya kujiajiri na kupata mitaji
kupitia mpango huo.
“Kwetu sisi Airtel tunaona
ni fahari kuwawezesha wajasiriamali kwa mafunzo na mitaji ili waweze kuendeleza
biashara zao na kukuza mitaji pia. Alisema Bayumi.
Ugunduzi wa gesi na mafuta mkoani hapa, vijana wanapaswa kujituma kwa kuongeza elimu na mitaji ili waweze kuwa sehemu ya wanufaika na kuondoka na hali ya kuwa watazamani wa tunu hiyo.
No comments:
Post a Comment