Tangazo

August 24, 2015

UN KUBORESHA VYOO VYA SHULE 10 KILIMANJARO

IMG_4176
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu, Moshi

MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.

Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.

Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.

Aidha aliwataka wanafunzi kuhakikisha kwamba wanajenga mshikamano mkubwa na wenye upendo kila kundi likithamini kundi jingine kwa ajili ya ustawi wa taifa .

Alisema wasichana kwa wavulana kuheshimiana kwani katika hilo wataweza kutengeneza taifa linaloheshimiana na hivyo kulinda msingi wa maisha wa amani unaowezesha maendeleo na ustawi wa jamii.

Aliwataka wanafunzi hao kushikilia ndoto zao na kusaidia kutambua kwamba wanahitajika kutunza mazingira na kujali afya zao.
IMG_4174
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem aliyeambatana na Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Kiboriloni.

Akimkaribisha Mratibu huyo kuzungumza na wanafunzi mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kiboriloni Salehe Msuya alisema kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1946 eneo la Msaranga na kuitwa kwa jina hilo na baadae kuhamishiwa Kiboriloni ambako kulikuwa na makazi ya Mangi mwaka 1955 inakabiliwa na ukosefu wa matundu 18 ya choo, maktaba na bwalo la chakula.

Alisema ingawa shule ilianzishwa ikiwa na wanafunzi 12 ilipohamishiwa Kiboriloni 1955 na kupewa jina hilo mwaka 1990, sasa ina wanafunzi 613 kuanzia darasa la awali hadi la 7 na kukabiliwa na changamoto za matundu.

Shule hiyo inahitaji kuwa na matundu 32 lakini yaliyopo sasa ni 14.
Mwalimu huyo aliishukuru UN kwa kuwasaidia kutengeneza matundu yaliyobaki na kuwaomba pia kusaidia kuboresha mazingira ya kusomea katika kuwa na maktaba na bwalo la kulia chakula.

Kwa sasa shule hiyo inatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wake na hawana mahali pa kulia.

Pamoja na taaluma kuzidi kuimarika shuleni hapo, shule haina maktaba.
IMG_4181
Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwasili kwenye eneo la tukio ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_4625
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuweka msingi wa ujenzi wa vyoo 18 ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira bora ya kusomea sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_4602
Sehemu ya wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni wakifurahi habari za kujengewa vyoo.
IMG_4159
Wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni wakinawa mikono yao kwa sababu mara baada ya kutoka msalani kama walivyokutwa na camera ya modewjiblog
IMG_4569
Baadhi ya vyumba vya vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4184
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) akiwapungia wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_4192
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akiweka maji wakati wa maandalizi ya kutengeneza zege kwa ajili ya kuweka msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakisubiri kuchanganya zege.
IMG_4198
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakianza matayarisho ya kuchanganya zege huku Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Martha Ofunguo akimwaga maji kwenye mchangayiko huo.
IMG_4207
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege.
IMG_4210
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakishiriki zoezi la kubeba maji na kokoto kwa ajili ya kuchanganya zege la msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4215
IMG_4217
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati akimwaga zege waliloandaa kwenye ujenzi wa msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4225
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakishiriki zoezi la kumwaga zege katika msingi huo.
IMG_4252
Hapa ni kazi tu.....; Ni maneno ya Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakati akishiriki zoezi la kuchanganya zege katika shule msingi Kiboriloni. Kwa matukio zaidi Bofya hapa

No comments: