Tangazo

September 14, 2015

Mh Iddi Azan azindua kampeni ya Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa kishindo!


Mh Iddi Azan akihutubia umti ulifurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar leo jioni.
Mh Iddi Azan leo hii alizindua kampeni ya ubunge wa jimbo la Kinondoni ambapo yeye ndiye mgombea aliyeteuliwa na CCM kuiwakilisha katika uchguzi mkuu unaotarajiwa kufanyikwa tarehe 25 ya Mwezi Oktoba 2015.

 Katika uzinduzi huo uliofana ambapouliopambwa na bendi maarufu ya Twanga pepeta na wasanii luluki akiwemo Tunda Man toka TIP TOP connection na Bonge la nyau, Mh Azan alielezea maendeleo yaliyopatikana katika muda ambao yeye amekuwa mbunge wa jimbo hilo ni pamoja na miundo mbinu ya ya barabara na afya ambapo ameahidi kuwa iwapo atchaguliwa tena kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha barabara zote kubwa zinatiwa lami kwa kuwa pesa tayari zimeptikamna toka world bank na atahakikisha wodi za kina mama waja wazito zinaongezwa ili kupunguza msongamano katika wodi hizo.

Uzinduzi huo pia ulishuhudia wanachama wawili nguli wa Chama cha wananchi CUF wakirudisha kadi zao na kujiunga na CCM kitendo ambacho kiliamsha hamasa kubwa miongoni mwa wanchama na wapenzi wa CCM chama tawala.
Mwenekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni akimnadi Mh Iddi Azan kwa maelfu ya watu waliohudhuria katika uzinduzi huo.
 Mstahiki meya wa wilaya ya Kinondoni Mh Yusuf Mwenda akiwapa vidonge Ukawa.

 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika viwanjani hapo.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge
Mgombea udiwani kata ya Mwananyamala Mh Songoro Mnyonge akaitambulishwa kwa wananchi
Mgombea udiwani wa kata ya Kijitonyama  Mh Kamugisha akitambulshwa na Mwenuekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni
Mgombea udiwani kata ya Tandale Bw Tamimu akitema vidonge kwa wapinzani.
Bw Massawe mgombea udiwani kata ya Ndugumbi.
 Mgombea Udiwani kata ya Magomeni, Ndugu Bujugo
Mwenekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni akipokea kadi ya CUF toka kwa bibi kada wa chama hicho ambaye alidai hajaona manufaa yeyote kuwepo katika chama hicho ambapo alijitoa rasmi na kurudi CCM.
Bibi akiwapungia mashabiki wa CCM baada ya kurudisha kadi ya chama cha wananchi CUF kwa mwenekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Nd Madenge.
Mzee Dalali akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao mwenyewe alidai umati ulifikia watu laki 250.









Wasanii wa kizazi kipya Tundaman na Bonge la Nyau wakitumbuiza mara baada ya Mkutani kwisha
Mh Iddi Azan akiaga mashabiki wake baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja vya  CCm Mwinjuma Mwananyamala leo hii jioni.

Picha na Geophrey Adroph habari na Mkala Fundikira

No comments: