Mmoja wa vijana Godlove Mato akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo
ya ujasiliamali toka kwa meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando, mafunzo
hayo yaliandaliwa na mradi wa kuwawesha vijana wa Airtel Fursa mkoni Dodoma
mwishoni mwa wiki. xxxxxxxxxxxxxx
Vijana nchini wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo
kupitia mpango wa Airtel fursa ulioanzishwa na kampuni ya simu za mikononi ya
Airtel wenye lengo la kuwawezesha wajasiriamali kujikwamua kiuchumi na
hatimaye kufikia malengo yao kimaendeleo.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika semina
ya wajasiliamali wadogowadogo iliyoandaliwa na Airtel mkoani Dodoma
kupitia mradi wake wa Airtel Fursa ambapo mwezeshaji wa semina hiyo
alikuwa Dokta Robert Mashenene ambae ni mtaalam wa maswala ya
ujasiliamaili na masoko na pia ni muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE
Dodoma.
“Vijana wa Tanzania wanapaswa kujituma zaidi
kutumia fursa kama zinazowazunguka na kuibuka na mbinu tofauti tofauti
kwa lengo la kupata ajira ndani yake na kuendeleza pato la nchi yetu
badala ya kulalamikia swala la ukosefu wa ajira mara kwa mara” alisema
Mashinene.
Akifundisha somo la ufafanuzi wa jinsi
yakusimamia wazo na amewataka watanzania kuachana na fikra potofu
za kudhani kwamba watu wanaofanikiwa kupitia kampuni hiyo wanakuwa
wameandaliwa na badala yake wachukue hatua ya kushiriki kwa kutuma
maombi yao kama inavyoelekezwa.
Kwa upande wake Mwalimu Chacha Magasi ambaye pia
ni mhadhiri kutoka Chuo Cha Biashara cha CBE mkoani Dodoma akisaidiana
na muwezeshaji huyo anawataka vijana wasomi na wa elimu ya chini
kujiajiri kwa kubuni biashara mbalimbali na kuchangamkia fursa ya
Airtel ili kupunguza tatizo idadi ya wahanga wa ukosefu wa ajira hapa
nchini kwa kuwa Airtel imeamua kuwawezesha na kuwapatia vitendea kazi
kupitia fursa.
“Pigeni hodi Airtel ombeni msaada wa fursa ili
kukamilisha dhamira ya kusimamia mawazo yenu na kupunguza wimbi la
vijana waliokosa ajira” alieleza Mwali Chacha.
Baadhi ya wajasiriamali 220 waliohudhuria
mafunzo hayo walisema Semina hiyo imesaidia sana kufungua fikra zao hasa
juu ya namna mafunzo hayo yalivyolenga kupanua uwezo wao mwingine wa
kujiajiri na sio kusubiria tu.
Nichoraus Sanga alisema mimi nimejifunza
kutosubiria tena ajira kuanzia kesho nakomaa na wazo langu la kujiajiri
kupitia kilimo cha zabibu na ufugaji wa samaki hapa Dodoma ni bidhaa
zinazohitajika sana.
Mradi wa Airtel fursa ni kwaajili ya vijana
nchini, Ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel Fursa
atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo
yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma
maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya
biashara.
|
No comments:
Post a Comment