Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto)
na Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel wakionyesha huduma mpya
ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kudownload application na kupata
huduma zote kwa urahisi kupitia simu zao .
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
* Huduma ya kwanza na kipekee kutolewa na kampuni ya mawasiliano ya simu nchini
* Inawawezesha wateja kupata huduma zote za
Airtel kwa urahisi
Dar es Saalam,
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel Novemba 24, 2015, imezindua application itakayowawezesha wateja
wake kupata huduma zote za Airtel kwa urahisi na kupitia application
ijulikanayo kama "Airtel care App".
Application hii mpya ya "Airtel care App" ni moja kati ya
huduma nyingi za kibunifu zinazotelewa na Airtel zenye lengo la kuwawezesha wateja wa Airtel kutatua matatizo yao na mahitaji yao kwa urahisi wakati
wowote.
Akizungumza Wakati wa uzinduzi wa "Airtel care App" Meneja Uhusiano
wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema " Airtel tumejikita katika kutafuta, kujua mahitaji ya wateja wetu kwa lengo la kubuni bidhaa na huduma
zinazokidhi na kutatua haja zao wakati wote.
"Airtel care App" inawawezesha wateja wetu, kuchagua kwa urahisi na kufanya
mambo mengi zaidi katika simu zao ikiwemo kuongeza salio, kuangalia salio, kuangalia matumizi na kiasi kilichosalia, kununua vifurushi
vya muda wa maongezi na intaneti, kutuma na kupokea pesa, kununua mlio wa sauti, kupata ripoti ya miamala ya pesa uliyofanya pamoja na
kupata msaada kwa watoa huduma. Huduma zote hizi zinapatikana kupitia application hiyo ya "Airtel care App"bila
gharama yoyote ya ziada.
Ili kupata "Airtel care App" mteja anaweza kupakua au kudownload Kupitia
Google Play kwa simu aina ya Android na kwa simu Iphone wanaweza kupata huduma hii kwa kupakua au kudownload application kwenye Apple
store.
No comments:
Post a Comment