Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akiteta
jambo na wafanyakazi wa Airtel wakati wa utambulisho wa program mpya ya
VSOMO.
|
Baadhi ya wageni wakifatilia utambulisho wa wa mpango huu
utakaowawezesha watanzania kusoma masomo ya ufundi yanayotolewa na VETA kupitia
simu zao za mkononi
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Mfumo wa kwanza wa
mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao Tanzania.
· Kuleta ufarahisi na
gharama nafuu.
· Mafunzo kupatikana
kupitia application maalum.
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA
imeshirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kuanzisha
application mpya ijulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, ili
kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA
nchini kupitia simu za mkononi . Kuanzishwa kwa VSOMO itasaidia kupanua wigo wa
mpango wa Airtel FURSA na kuwafikia vijana wengi zaidi nchini.
Akiongea kuhusu
uhusiano huo, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso alisema” tumeona ni
muhimu kuwekeza kwenye mpango huu wa VSOMO kwa kuwa tumeona vijana wengi wana
kiu na haja ya kutaka kujifunza na kuhitimu mafunzo ili kukuza biashara zao na
kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri. Matumizi ya simu za kisasa yanakuwa
kila siku, mpaka sasa takribani wateja milioni 10 wanatumia simu za kisasa na
kati yao 70% ni vijana. Hivyo VSOMO itawafikia vijana wengi zaidi nchini kwa
urahisi zaidi.Na ndio maana tunauza simu zetu kwa bei ndogo ya hadi Tshs elfu
80,000/=kuhamasisha mafunzi kwa kupitia njia ya simu za mkononi”.
“Tunaamini ushirikiano
huu kati ya VETA na Airtel FURSA utawawezesha mamilioni ya vijana wakitanzania
kupata mafunzo ya ufundi yanayotolewa na VETA wakati wowote na mahali popote
kupitia simu zao za mkononi. Tunauhakika application hii ya VSOMO
itachochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha kuwa na
wafanyabiashara na wafanyakazi bora walio na nyenzo zinazohitajika katika
kuleta ufanisi”. Aliongeza Colaso
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bwana Geoffrey G Sabuni alisema “ nafurahi kuwa sehemu
ya utambulisho wa kihistoria wakuanzishwa kwa mafunzo ya ufundi kwa njia ya
simu yenye lengo la kuwapatia watanzania nafasi ya kujiunga kwa wingi katika
stadi za ufundi. Bwana Sabuni aliwapongeza timu nzima iliyoshiriki katika
kuanzisha ubunifu huu wa VSOMO na kusema ni jambo litakalowezesha watanzania
kwa mara ya kwanza katika historia ya ufundi stadi kuweza kuwa wataalamu
watakaopeleka nchi katika uchumi wa kati. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA
alisisitiza VSOMO inaendana na malengo ya VETA ya kuongeza idadi ya wanafunzi
wanaojifunza mafunzo ya ufundi na hivyo kufanya vizuri kwa mafunzo haya kwa
hatua hii ya awali kutapelekea kutanua wigo zaidi ili kufikia vijana wengi
zaidi
Kwa upande wake Mkuu wa
chuo Veta Kipawa, Eng. Lucius Luteganya alithibitisha kuwa Mafunzo kwa njia ya
mtandao yamezoeleka sana duniani lakini kwa Tanzania hii ni mara ya
kwanza kuanzishwa kwa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao. Kila mwaka VETA
inapokea maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali toka kwa vijana zaidi ya elfu 15
nchini na theluthi tatu ya maombi hayo ndo yanayokubaliwa na kupokelewa
katika vituo vyetu nchini na kuacha theluthi mbili bila kupata fursa ya mafunzo.
VSOMO kwa kiasi kikubwa kitaongeza uwezo wetu wa kufundisha watanzania wengi
zaidi hususani vijana hivyo kuongeza idadi ya watu wenye ujuzi na
kuchochea uchumi wa nchi kukua kwa kasi zaidi, alisema Luteganya
” ili kuhakikisha
tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA, Eng. Luteganya aliongeza
kwamba “ wale wote watakaojiunga na VSOMO watatakiwa kufanya mtihani ili
kufudhu mafunzo ya vitendo yatakayotolewa na VETA katika vituo vyao nchi nzima.
Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale watakaofaulu mafunzo katika
hatua zote mbili ya nadharia na vitendo. Alithibithisha.
Akiongea kuhusu mpango
wa VSOMO, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya
alisema “mafunzo kwa njia ya mtandao ni rahisi na yatapatikana kwa
wateja wa Airtel wenye simu za aina ya android. Mteja atatakiwa kupakua
ya VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na
kujiandikisha bure bila gharama zozote. Mara baada ya kumaliza
masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo
karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua
muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60 na ndipo atakapokaa
kwajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza
Singano alisema” Mwanafunzi
atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa kulipia kiasi cha ada yenye
punguzo shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60#..
Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya
ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”
No comments:
Post a Comment