Tangazo

July 4, 2016

Airtel na VETA wawafikishia VSOMO vijana wa mkoa wa Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Mwanza katika kijiwe cha waendesha bondabonda wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza. Pichani ni wafanyakazi wa Airtel na VETA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella akimpatia vipeperushi mmoja wa kijana katika kijiwe cha Bodaboda mkoani Mwanza wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza.
Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella mara baada ya kumtembelea ofisini kwakwe na kutambulisha fursa zinazopatikana kwa wakazi wa mwanza kupitia mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi ujulikanayo kama VSOMO unayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel
 XXXXXXXXXXXX
MWANZA

MPANGO maalumu wa VSOMO unaotolewa kwa ushirikiano kati ya Airtel na VETA unalenga kuwafikia vijana wengi zaidi katika kila kona ya nchi kupitia simu za mkononi hivyo kuwapa urahisi wakazi wa mwanza na maeneo mengine kupata nyenzo na mbinu muhimu katika biashara zao na kuwaandaa vyema katika ushindani wa ajira ili kuinua uchumi wa viwanda wa Tanzania

Akiongea na wakazi wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  aliwapongeza VETA na Airtel kwa kuanziasha mpango huu wa VSOMO kwa wakati muafaka.  Alisema “mpango huu ni wakibunifu na umekuja wakati muafaka kwani utawawezesha vijana kupata masomo ya kiufundi ambayo yachochea kukua kwa uchumi wao. Hivyo nawaomba VETA na Airtel  wahakikishe VSOMO inaendelea kuwa mpango bora utakaosaidia watanzania kupata vijana wengi wenye taaluma kwaajili ya kuendesha uchumi wa viwanda na kunufaika na ajira zitakazotokana na kufanya vizuri kwa viwanda hivyo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza alitoa wito kwa vijana wa mkoa huo kutumia fursa hii kwa kujiunga na masomo ya VETA kupitia VSOMO. Alitoa shukrani zake  na kusema “ Tunafurahi kwa Mwanza kuwa kati ya mikoa iliyopata nafasi ya kushuhudia uzinduzi huu kati ya VETA na Airtel. Nawapongeza kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunawawezesha watanzania kupata elimu bora na ujuzi zaidi  kupitia VSOMO.

Kwa upande wake, Meneja huduma kwa jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema  “ katika kutekelea za huduma zetu za jamii kwa nchini Airtel imedhamiria kuwawezesha na kuwaendeleza vijana kujikwamua kiuchumi kupitia program zetu. Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutengeneza suluhisho  la kibunifu kupitia simu za mkononi  ambalo limeleta tija kwa jamiii kama vile VSOMO kwaupande wa msomo ya ufundi kwani VSOMO inawawezesha wateja wa Airtel kupata ujuzi na maarifa kupitia viganja vyao”

Akiongea kuhusu VSOMO,  Mkuu wa chuo cha VETA kipawa Eng. Lucius Luteganya, alisema “ kuanzishwa kwa mfumo huu wa VSOMO kutachochea mabadiliko makubwa yatakayotoa nafasi kwa watanzania kutumia mpango huu wa kipekee kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na kwa gharama nafuu mahali popote kwa kutumia simu zao. 

Huu ni mpango wa kipekee Afrika mashariki na kati kwa kuwa hakuna taarifa zinazoonyesha mfumo kama kuna application yenye kutoa  mafunzo ya ufundi duniani. wazi kabisa kukuwa kwa uchumi wa viwanda kutazidi kukua kutokana na upatikanaji wa elimu za ufundi kwa uhakika na urahisi na hivyo kushukuru kwa ushirikiano ulianzishwa kati ya VETA na Airtel unakaosaidia utekelezaji wa mpango wa viwanda  wa serikali  ya awamu ya 5

Kozi vinazotolea kupitia application ya VSOMO  kwa sasa ni pamoja Misingi Ya Ufundi Wa Pikipiki, Kuweka Umeme, Ufundi Wa Simu, Kuchomelea Na Kuunda Vyuma na Urembo Kozi hizi zinatolewa kwa gharama ya shilingi 120,000, muda wa kufanya mafunzo ya vitendo baada ya kufaulu masomo kwa njia ya mtandao ni masaa 60. Hii inamaanisha kwa aliyedhamiria kushoma itamchukua mwezi moja kumaliza masomo yake kupitia VSOMO.


No comments: