Tangazo

September 21, 2016

RC KILIMANJARO SAID MECKY SADICK ATEMBELEA KIWANDA CHA TANGAWIZI

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wake wa kazi alipozuru wilaya ya Same
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Same kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki
 Wananchi wakisikiliza kwa makini mkutano wa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro


Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki akitoa salamu kwa wajumbe wa kamati ya ulizni na usalama na salamu za kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadickalipotembelea Wilayani hapo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadickakikagua mashine katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akipokea maelezo kuhusu mashine hizo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadickalipokagua mfereji wa Mshana

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick amezuru katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same.

Sadick ametembelea kiwandani hapo akiwa ba dhamira ya kukifufua kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi ya izalishaji katika kiwango cha juu ili kwenda sawia na kasi ya Maendeleo inayohitaji kwa wananchi wa eneo hilo sambamba na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho pia unapaswa kutunza vyanzo vya maji lakini pia kuchemsha maji ya kunywa ili kuepukana na Maradhi mbalimbali yatokanayo na unywaji wa maji yasiyo safi na salama.

Katika sekta ya elimu amesema kuwa ni dhahiri kuwa miundombinu ya shule inapaswa kuboreshwa ili waalimu wakae kwenye vituo wanavyopangiwa na kuachana na tabia ya kuhamahama.

Rc Sadick amezungumzia pia mimba za utotoni ambapo amewataka wananchi kuwaacha watoto wa kike waweze kusoma ili baadae wasiwe tegemezi tofauti na ilivyo sasa anbapo wazazi wengi wanawaozesha wabinti wakiwa na umri mdogo jambo ambalo ni kinyume kabisa na utaratibu wa ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.

Kabla ya mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same walifanya mazungumzo na Bodi ya uongozi wa Ushirika wa kiwanda hicho na kuwataka waongeze juhudi kuhakikisha wakulima wa Tangawizi hawapati hasara tena.

Rc Sadick ameutaka uongozi wa viwanda vidogo vidogo SIDO ambao ndio wenye mitambo iliyofungwa kiwandani hapo kuboresha mashine hizo ambazo kwa sasa zinatumia OIL chafu kuhamia kwenye umeme ili kiwanda kiwe rafiki kwa mazingira pia.

Zao la Tangawizi linalimwa sana katika Kata hiyo ya Miyamba hivyo kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaleta mapinduzi makubwa katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

No comments: