Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa
Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa
Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya
Tanga.
Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar
es salaam, Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na
Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali
na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri,
Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu
ya makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari
katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka
jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la
mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga,
Tanzania. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment