NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WANANCHI
binafsi wanaweza kwenda kwenye mabenki na kuomba mikopo ya fedha za ujenzi, (Mortgage
Finance), bila ya kuanza kupitia kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi-Usimamizi wa Mabenki Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Eliamringi Mandari, (pichani juu), wakati
akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa mikopo ya fedha kwa ajili ya ujenzi,
(Mortgage Finance) na utunzaji taarifa mteja (mkopaji) katika kitunza taarifa
cha kibenki, (Databank) kwenye semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha
leo Machi 29, 2017 inayoendelea kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (tawi la
Zanzibar), mjini Unguja.
“Watu
wengi hawajui kama kuna fursa hii ya ku-mortgage, kwa maana ya kujenga, kununua
au kurekebisha nyumba yako, na katika kudhamiria kufanya hayo, benki inaweza
kutoa masharti ambayo ni ya kurejesha fedha (mkopo) huo kwa muda mrefu kati ya
miaka 5 hadi 20.” Alisema.
Hata
hivyo alisema kama ilivyo kwa masharti mengine yahusuyo kukopa, hata fursa hii
ya kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi vigezo na masharti pia huzingatiwa ili
benki iweze kutoa mkopo huo.
Aidha
kuhusu mfumo wa taarifa unaosaidia mkopeshaji,(lender), kumjua mkopaji,
(borrower), ujulikanao kama, Credit
Reference System, (DBS), alisema Sheria namba 48 ya BoT kuhusu masuala ya
kubadilishana taarifa za mikopo, kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha inalazimisha
mabenki na taasisi hizo kutuma taarifa za wateja (wakopaji), kwenye Databank ya
BoT kila mwezi, alisema Bw. Mandari
Alisema pia BoT, inaandaa utaratibu
utakaolazimisha wakopeshaji binafsi na Taasisi za Kibinafsi, (NGOs),
zinazojihusisha na utoaji mikopo, kusimamiwa, (Regulated), katika utoaji wa
taarifa za mteja (mkopaji), katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank), ili
kuwaondolea usumbufu wananchi.
“Ni kweli Sheria inaitaka Benki Kuu kusimamia taasisi za fedha
zinazochukua amana kutoka kwa wananchi, kwa kuwasilisha taarifa hizo za
wakopaji kwenye mfumo huo wa BoT wa Databank, lakini kwa sasa wakopaji binafsi
na taasisi za hiari zinazojishughulisha na utoaji mikopo ya kifedha, bado sera
inaandaliwa ili na wao waweze kusimamiwa.” Alisema.
Alisema,
wakopaji binafsi na NGOs zinazojihusisha na utoaji mikopo, zimekuwa zikitumia
mabavu wakati mwingine katika kufuatilia marejesho ya mikopo kutokana na
utaratibu usio wazi wa kukopa, na wakati mwingine wakopaji wanarejesha mikopo
kwa riba kubwa, alifafanua.
Bw. Eliamringi Mandari, akiwasilisha mada hiyo
Meneja Msaidizi Msoko ya Ndani wa BoT, Bw.Genes Kimaro, akiwasilisha mada juu ya Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa Sera ya Fedha wa BoT.
Bw.Genes Kimaro
Mchambuzi wa Masuala ya Fedha wa BoT, Bw.Mohammed Kailwa, (kushoto), akijibu baadhi ya hoja wakati akisaidiana na Meneja wa Masoko ya Ndani, Kurugenzi ya Masoko ya Fedha (BoT), Bw.Reverian Felix
Baadhi ya waandishi wa nhabari za Uchumi na Fedha wanaohudhuiria semina hiyo
Meneja wa Fedha na Utawala, Bodi ya Bima ya Amana ya BoT, Bw. Richard Malisa, akitoa mada jinsi Bodi ya Bima ya Amana inavyokinga amana za wananchi |
Mwandihi wa Clouds TV, Bw. Austin Beyadi, (kulia), akihariri habari wakati semina ikiendelea. Kushoto ni Grace Semfuko wa Star Tv.
Mmiliki wa Mtandao wa TZ Business News Online, Jaston Binala, akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT Bw. Lwaga Mwambande, (kulia), akifafanua jambo wakati wa semina hiyo
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina, (kushoto), akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari Zanzibar, (ZBC), wakati wa mapumziko ya mchana ya semina hiyo.
Mwenyekiti wa Semina, ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Raia Mwema, Bw. Ezekiel Kamwaga, akizungumza kwenye semina hiyo
Bi. Vicky Msina, (kulia), na Bw. Lwaga Mwambande kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, wakifuatilia mijadala na mada zilziokuwa zikitolewa
Bi. Vicky (kulia), akiwa na Bi. Flora Mkemwa kutoka Idara ya Uhusiano na Itifaki BoT
Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, akifuatilia mjadala.
No comments:
Post a Comment