Tangazo

June 23, 2017

DC TEMEKE MHE FELIX LYAVIVA AWAAGIZA WAKURUGENZI JIJINI DAR ES SALAAM KUANZISHA DAFTARI LA WAKAZI KILA MTAA

MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe Felix Lyaviva akizungumza wakati wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akitoa maelezo kuhusu semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe Felix Lyaviva akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mrakibu msaididzi wa Polisi Makao Makuu kitengo cha Makosa ya mitandao Joshua Mwangasa Akielezea takwimu na jinsi ya kudhibiti makosa ya mitandao ya kijamii nchini.
Meya wa Manispaa ya Ubungo Ndg Boniface Jacobo (Kulia) akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni Bi Gift Msuya akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Theresia Mbando akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita akitoa mtazamo wake wakati wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini

Na Mathias Canal, Dar es salaam

MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe Felix Lyaviva amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo kuanzisha daftari la wakazi katika kila Mtaa katika Jiji la dar es salaam.

Alisema kuwa ili kupunguza uhalifu katika Mkoa wa Dar es salaam ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Jiji hilo na mahali wanapofikia.

Ametoa agizo hilo wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.

Katika Semina hiyo wadau wamekumbushwa namna ya kuelewa Zaidi hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji, Umuhimu wa anuani za makazi na Post-kodi kwa maendeleo ya Taifa, Faida za huduma ya kumiliki na kuhama na namba ya simu ya kiganjani na mwelekeo wa Teknolojia na huduma za mawasiliano na utangazaji hapa nchini.

 Mhe Lyaviva alisema kuwa pamoja  na faida kubwa inayopatikana kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini ambayo inawezesha ukuaji wa kasi wa sekta nyingine, kumekuwepo na watu wachache katika jamii ambao wanatumia fursa hiyo vibaya hivyo kusababisha usumbufu kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla.

Alisema kuwa wapo wanaotumia simu na mitandao ya kijamii kupanga mikakati ya uhalifu huku wengine wakitumia simu na mitandao hiyo kukashifu na kutukana watu wengine.

Mhe Lyaviva alisema kuwa lengo la serikali ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya Mawasiliano na utangazaji ili kutoa fursa za ajira na kuwezesha huduma hizo kuwafikia wananchi wote kwa gharama nafuu.

Naye Mrakibu msaididzi wa Polisi Makao Makuu kitengo cha Makosa ya mitandao Joshua Mwangasa akiwasilisha mada kuhusu makosa ya mitandao ya kijamii alisema kuwa kuna njia nyingi zinazotumiwa ili kufanya uhalifu ikiwemo mitandao ya kijamii hivyo amewasihi watumiaji wote wa mitandao ya kijamii nchini kubadili mara kwa mara Namba za siri (Password).

Alisema kuwa kufanya hivyo ni miongoni mwa njia nzuri ya kuepuka kuingiliwa na wahalifu katika mawasiliano yao kwani kwa kiasi kikubwa maisha ya binadamu yanaenda kubadilika kutokana na teknolojia

Akitoa takwimu na jinsi ya kudhibiti makosa hayo kwa viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, Mwangasa alisema kuwa Mwaka 2016 makosa ya mitandao ya kijamii yameongezeka kufikia 9441 ukilinganisha na Mwaka 2015, ambapo amezitaja sababu za kuongezeka kwake kuwa ni pamoja na ongezeko la uelewa wa wananchi na hatimaye kutoa taarifa za matukio hayo katika vituo mbalimbali vya Polisi nchini.

No comments: