Godfrey Magila kutoka taasisi ya DTBi akitoa mada wakati
kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa
kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO.
Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi
XXXX
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA wameshiriki kongamano la elimu kupitia
mtandao yenye lengo la kuhamasisha ubunifu kwa vijana na kuonesha jinsi
kijana anavyoweza kusoma kwa kujitengemea kwa kutumia ubunifu wa
aplikesheni ya VSOMO inayotoa elimu kwa mtandao.
Kwa miaka miwili sasa, VETA kupitia applikesheni ya VSOMO imekuwa
ikitoa elimu kupitia mtandao kwa wanafunzi ambao wanataka kupata elimu ya
ufundi stadi kwa udhamini wa Airtel Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kongamani hilo,
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kampuni ya
Airtel iliamua kuwa mmoja wa wadau wa teknolojia hii ya kutoa elimu ya VSOMO
ikiwa ni moja wa mkakati wake wa kurudisha sehemu ya faida yake katika kusaidia
Jamii.
Kwa kuweza kutambua umuhimu wa Jamii inayotuzunguka, tuna miradi ya
kusaidia vijana kujikwamua yenye lengo ya kuwapa vijana ujuzi ili wajiajiri au
wapate ajira kwenye sekta mbali mbali ili kuunga mkono juhudi za serikali za
kujenga uchumi wa viwanda.
Airtel Tanzania inayo furaha kuona kuwa matumizi ya smartphone
yakiwa ni darasa au ikiwa ni moja ya njia ya kutumika kupata elimu ya ufundi.
Hii haiukuwa rahisi kufanya peke yetu ndio sababu tuliamua kushirikiana na VETA
kama taasisi ya serikali yenye mamlaka ya kutumia elimu ya ufundi hapa nchini
huku DTBi wakiwa ndio waliombuni applikesheni ya VSOMO, alisema Singano.
Airtel na washirika wake VETA na DTBi kwa sasa wana utaratibu mpya
wa malipo kwa awamu ili kuwezesha wanafunzi wanaotaka kupata elimu ya ufundi
stadi kufanya bila kupata changamoto za kulipa karo, aliongeza Singano.
Mkuu wa chuo cha VETA Kipawa Injinia Sospeter Dickson Mkasanga
alisema kuwa teknolojia imekuwa sana katika dunia ya leo na Tanzania kama nchi
pia imefaidika sana. Kwa kutumia teknolojia, kila kitu sasa kinawezekana. Ni
kwa kutumia teknolojia tumeweza kutoa elimu ya ufundi stadi kwa zaidi ya vijana
100 wakiwa hawapo darasani. Hii ni kitu ya kujivunia kwa sababu vijana hao
wameweza kujiajiri na wengine wameajiri kwenye sekta mbali mbali kwa
tunawakabidhi vyeti baada ya kumaliza elimu yao, alisema Mkasanga.
VSOMO imeweza kuwa mkombozi wa elimu ya ufundi stadi kwa kutumia
teknolojia. Kwa kutumia simu za smartphone, wanafunzi wanapata ufundi
stadi wa kozi yeyote wayohitaji. Naomba nitoe wito kwa vijana wote nchini ambao
wangependa kupata elimu ya ufundi stadi wajiunge na wapakue applikesheni ya
VSOMO kwani ni rahisi na pia malipo ya kozi ni nafuu, aliongeza Mkasanga.
Kwa upande wake,
Godfrey Magila kutoka DTBi alisema kuwa ili kufanya teknolojia iwe na tija kwa
Jamii, ni muhimu kwa Jamii kupata elimu ya umuhimu na matumizi ya teknolojia
ili kufaidika nayo na pia kufanya baadhi ya mambo yawe rahisi katika maisha
yao.
Jamii zetu zinapata changamoto kufikia malengo
yao. Kwa sasa, teknolojia imekuwa kwenye vidole vyetu na ndio sababu watu wengi
wanatumia smartphone ambazo zina uwezo wa kuweka memori kubwa. Kama Jamii yetu
ingeweza kutambua na kuelewa elimu iliyopo kwenye smartphone hizo ingekuwa ni
jambo la maana, alisema Magila.
Tangu kuzinduliwa
kwa VSOMO Juni 2016, inaonyesha kuwa zaidi ya vijana 30,000 washapakua
applikesheni ya VSOMO huku zaidi ya 10,000 wakijisajili na zaidi ya 100 wakiwa
tayari washamaliza kusoma kupitia applikesheni hiyo na kukabidhiwa vyeti vyao.
Kozi ambazo
ulitolewa ni pamoja na Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja,
Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme
wa magari, Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za
mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma
Ufundi wa kuchomea vyuma.
No comments:
Post a Comment