Tangazo

May 23, 2018

WATANZANIA WENGI HAWAFAHAMU KUFANYA MANUNUZI KWA NJIA YA MTANDAO

Na Jumia Tanzania

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, biashara nyingi Tanzania na duniani kote zimehamia kwenye mifumo ya mtandao wa intaneti. Ni miongoni mwa sekta inayokua kwa kasi hivi sasa ikiwa imechangiwa na kuendelea kubadilika kwa tabia za wateja kila kukicha wakiwa na mahitaji mapya. 


Biashara kupitia mtandao wa intaneti inawaruhusu wateja kubadilishana taarifa mbalimbali juu ya huduma na bidhaa zinazouzwa mtandaoni kukiwa hakuna vikwazo vya muda au umbali. Inatarajiwa kuwa ndani ya kipindi cha miaka michache ijayo, makampuni mengi yatakuwa yamehamishia huduma zao katika njia ya mtandao. Wataalamu wanapendekeza kuwa, endapo biashara kwa njia hii zikifanyika kwa usahihi zina manufaa makubwa ikiwemo; uharaka, unafuu, na ni rahisi zaidi ukilinganisha na njia za kawaida zilizozoeleka.    


Tumekuwa tukishuhudia wafanyabiashara wengi wakitangaza kuhusu bidhaa na huduma wanazozitoa kupitia njia mbambali za mitandaoni kama vile Facebook, Twitter na Instagram. Wengi wao wamekuwa wakiwataka wateja wao kutembelea kurasa zao na kuchagua bidhaa zao kisha wapelekewe mpaka walipo. Lakini je, hii ndio maana halisi ya biashara kwa njia ya mtandaoni?


JUMIA ni kampuni inayojishughulisha na biashara tofauti kwa njia ya mtandao wa intaneti barani Afrika, ambapo kupitia tovuti yake huwakutanisha wauzaji na wanunuzi mbalimbali kwa urahisi. Kupitia tovuti yake, maelfu ya wauzaji na wanunuzi wanaweza kufanya biashara bila ya kuonana isipokuwa kubadilishana taarifa. 



Kwa mfano, mteja akiingia kwenye mtandao huu anachoweza kukiona ni orodha ya bidhaa nyingi kutoka kwa wauzaji tofauti, akachagua anazohitaji, akajaza taarifa zake binafsi, akachagua njia ya malipo na hatimaye kutaarifiwa ni lini mzigo wake utamfikia. Kumbuka, mlolongo wote huo unaweza kufanyika bila ya mawasiliano au kuonana uso kwa uso baina ya pande zote mbili.  


Makala haya yamejaribu kuangazia kuhusu uingiaji wa sekta hii nchini Tanzania na namna ilivyopokewa na wateja. Miongoni mwa mambo yatakayozungumziwa humu ni pamoja na nafasi ya kitengo cha huduma kwa wateja katika kutoa huduma na elimu kwa wateja. 


Akifafanua umuhimu wa kitengo cha huduma kwa wateja cha Jumia Tanzania, Mkurugenzi Mkuu, Bw. Zadok Prescott ameelezea kuwa wateja wengi bado hawafahamu huduma zinazotolewa na kampuni yake ukilinganisha na makampuni mengine yanayojihusisha na biashara za mtandaoni nchini Tanzania. 




“Jumia ni tovuti PEKEE ya biashara mtandaoni Tanzania inayomhakikishia mteja bidhaa mpya na halisi (orijino), au kurudishiwa pesa yake kama haitokuwa hivyo. Mteja akishafanya huduma mtandaoni na kujaza taarifa zake hupelekewa bidhaa zake mpaka alipo, ndani ya siku chache tu mara ya baada ya kufanya huduma. Pia ni tovuti PEKEE ya biashara mtandaoni Tanzania unayoweza kulipia pindi unapofikiwa na bidhaa yako kwa jijini Dar es Salaam, hivyo ni salama kwa mteja endapo atakuwa na hofu ya kutapeliwa. Kama haitoshi tunawaruhusu wateja kurudisha bidhaa bila ya makato yoyote, kama ni kinyume na walivyoagiza,” alifafanua zaidi Prescott.


Ni dhahiri kwamba Watanzania wengi bado ni wageni na teknolojia za kisasa hususani hii ya kufanya biashara kupitia mtandao wa intaneti. Miongoni mwa wengi wao wamezoea kwenda moja kwa moja dukani na kununua bidhaa wanazotaka au watakazoziona. Kwa hiyo hapa mteja anakuwa na fursa finyu ya kuonana na wauzaji mbalimbali kwa sababu itamlazimu kutumia muda mwingi.


Akifafanua hilo, Bw. Prescott amesema kuwa Jumia inayo timu maalum ya huduma kwa wateja. Timu hiyo imejikita katika kuwasaidia wateja kufanya na kufanikisha huduma kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya mwisho. Kwa sababu wanafahamu kuwa wapo Watanzania wengi bado hawajajaribu kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Na kuna uwezekano wengine walipojaribu kufanya hivyo walitaka kutapeliwa.


Amesema kuwa wameaona ni vema kuwa na timu hiyo kwa sababu wateja wengi hawana imani huku wengine wakiwa na hofu. Wengi wao bado wanaamini hawawezi kununua bidhaa bila ya kuiona kwa macho, kuikagua na kujiridhisha na pengine mpaka kuijaribisha kabisa.



“Kama walivyo wateja wengine duniani, Watanzania pia huzingatia bei pamoja na ubora. Wanahitaji bidhaa bora zenye bei nzuri na zinazowafikia kwa njia rahisi. Lakini kikubwa na cha msingi ni uaminifu. Haya ndiyo masuala ya msingi yanayozingatiwa na Jumia ambayo hayapatikani kwa kampuni zingine Tanzania.”



Kutokana na wateja wengi kujizoesha utamaduni huo, Jumia inakumbana na changamoto ya wengi kutokuwa na imani na mitandao inayoibuka kila kukicha. Katika kuhakikisha wanaaminiwa na wateja wake Jumia hufanya yafuatayo:   


“Watanzania bado hawaitumii ipasavyo huduma bora za manunuzi na uuzaji zinazotolewa na Jumia. Wengi wao bado wanashindwa kutofautisha kati ya kampuni ya biashara mtandaoni iliyojikamilisha kama Jumia, na mitandao mingine ya kawaida ambayo kila mtu anaweza kuuza na kununua bidhaa. Tofauti ya Jumia na mingineyo ni kwamba, mteja anapaswa kulipia bidhaa pale inapomfikia, tena ikiwa halisi na ubora alioutarajia.”


“Tunachoweza kuwaahidi wateja wetu ni kuwapatia idadi kubwa ya bidhaa tofauti kwa bei nzuri na kuwafikishia pale watakapohitaji,” aliongezea na kumalizia Bw. Prescott, “Jumia imejikita zaidi katika kuokoa MUDA na PESA kutoka kwa wateja wake - bidhaa adimu kabisa duniani!” 

No comments: