Tangazo

August 17, 2011

Nyota wa Kikapu Marekani Dwight David Howard aipiga 'Jeki' Sekondari ya Kipok Monduli

Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akimpokea Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Orlando Magic ya nchini Marekani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya D12 Foundation ya nchini humo, Dwight David Howard wakati alipokuwa akiwasili jimboni humo juzi.
Dwight Howard akipungia mikono wakazi wa Monduli mara baada ya nyota huyo kutembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kipok iliyopo Wilayani Monduli na kutoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni  90  kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafuzi shuleni hapo.
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Orlando Magic ya nchini Marekani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya D12 Foundation ya nchini humo, Dwight David Howard akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 90 kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kipok, Felister Lukumay kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafuzi shuleni hapo. Anayeshuhudia (katikati) ni Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa.

No comments: