Tangazo

September 2, 2011

Tamasha la Epiq Nation 'lawasha moto' Coco Beach - Eid El Fitr

Kundi la TMK Wanaume Halisi likitumbuiza maelfu ya watu waliofika katika Tamasha kubwa la Epiq Nation lililoandaliwa na kampuni ya Zantel ikiwa ni katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitr kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Dj Mafuvu wa East Africa Television & Radio (katikati) akionyesha utaalamu wake wa kupiga 'Beat' yaani midundo ya muziki kwa mdomo huku akisindikiwa na watangazaji wa EATV & Radio.
Msanii wa Original Comedy ya EATV, Massawe akifanya vitu vyake.
Umati wa watu waliofurika katika tamasha hilo.
Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Halisi, Juma Kassim Kiroboto ' Sir Nature' (katikati) akicheza sambamba na waimbaji wake, Mabaga Fresh (kushoto) na YR.
Mkali wa miondoko ya Hip Hop nchini, Roma Mkatoliki naye alikuwepo.
Wachafua hali ya hewa huwa hawakosekani sehemu kama hiii..
Ambwene Yessaya 'AY' alitoka sambamba na Nyota wa wimbo wa kigeugeu kutoka Kenya, Jaguar (kulia).
Mfalme wa Muziki wa Bongo Crunk, C- Pwaa akiimba sambamba na wacheza shoo kutoka Norway, Emilie Asla (kushoto) na Otilie Pettersen (kulia) wakiwajibika jukwaani ipasavyo.
C- Pwaaaaaaaaaa.... Picha zote/John Badi wa Daily Mitikasi Blog

No comments: