Tangazo

December 30, 2011

JESHI LA POLISI MKOA WA MOROGORO LIMETOA MSAADA WA VYAKULA KATIKA KAMBI YA WAZEE FUNGA FUNGA.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa morogoro, Adolphina Chialo akizungumza na wazee wa Kituo cha Funga Funga katika Kata ya Kichangani mkoani Morogoro kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula.

Kamanda Chialo akimkabidhi sehemu ya msaada kwa mtoto, Rose Juma (12).


Hapa Kamanda Chialo akimkabidhi, Seleman Kisengo (12) ambapo watoto hao ni miongoni mwa watoto wanaoishi katika kambi hiyo ya wazee wasiojiweza ya Fungafunga.
Sehemu ya wazee wasiojiweza wa kituo hicho wakimsikiliza kamanda Chialo. Picha hisani ya Juma Mtanda Blog

WADAU HAYA NI MATENDE AUUUU....? MSAADA


Auric Air yajitosa Tabora Livingstone Marathon

Meneja Maendeleo ya Biashara wa Auric Air, Deepesh Gupta (kushoto) akikabidhi msaada wa fulana kwa Mratibu wa mashindano ya mbio za Tabora Livingstone Marathon, Ramadhani Makula jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Uratibu wa mbio hizo, Tullo Chambo. 

                                    ******************************************
 
Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Ndege ya Auric Air ya jijini Dar es Salaam imejitosa kusapoti mashindano ya Mbio ya Tabora Livingstone Marathon yanayotarajiwa kufanyika mjini Tabora Machi mwakani.


Mbio hizo za kwanza katika historia ya Mkoa wa Tabora, zitakuwa za Nusu Marathon Kilomita 21 na zile za kujifurahisha za Kilomita 5.


Akikabidhi msaada wa fulana kwa Mratibu wa mbio hizo, Ramadhani Makula jijini Dar es Salaam jana, Meneja Maendeleo ya Biashara wa Auric Air, Deepesh Gupta, alisema, wamesukumwa kutoa msaada hyo ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu nne chini ya Rais Jakaya Kikwete katika kuendeleza na kuhamasisha michezo hapa nchini.


Gupta alisema, kwa kuzingatia malengo na madhumuni yam bio hizo, wameona japo watoe msaada huo mdogo wa fulana zitakazotumiwa na waratibu na wasimamizi wa mbio hizo ili kusaidia kufanikisha tukio hilo muhimu.


Akipokea msaada huo, Mratibu wa Tabora Livingstone Marathon, Makula, aliishukuru kampuni hiyo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwaunga mkono katika kufanikisha mbio hizo za kihistoria.


Makula alisema, hafla ya uzinduzi rasmi wa mbio hizo ambao utawashirikisha wadau na wafadhili mbalimbali utafanyika jijini Dar es Salaam Januari 10.


Aliwataka vijana wenye vipaji mbalimbali wa Mkoa wa Tabora na maeneo ya jirani kujiandaa na mbio hizo, huku akitoa pongezi kwa ushirikiano unaotolewa na Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora.

RAIS KIKWETE ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MTANGAZAJI WA TBC, MAREHEMU HALIMA MCHUKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO

Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Mtangazaji Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa. PICHA NA IKULU

Rais Jakaya Kikwete akiwapa pole wafiwa.

Rais Jakaya Kikwete na waombolezaji wakiombea mwili wa Halima Mchuka.


Sehemu ya ndugu, jamaa na wadau mbalimbali waliofika kumuaga Marehemu Malima Mchuka. Mwenye suti nyeusi ni aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Tido Mhando

TASWA yatoa Pole kufutatia Vifo vya Wanahabari, Halima Mchuka na John Ngahyoma

Katibu Mkuu Taswa, Amir Mhando
. Pia Kufanya Marekebisho Madogo ya Katiba


(A) MAREKEBISHO YA KATIBA

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ilikutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ilikubaliana kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho ili iendane na wakati wa sasa.

Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji imemteua mwanamichezo maarufu ambaye pia ni mwanasheria na wakala wa wachezaji wa soka, Damas Ndumbaro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho  ya Katiba ya TASWA.

Wajumbe wengine kwenye kamati hiyo ni George John ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa TASWA, Alfred Lucas ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA na Amir Mhando ambaye ni Katibu Mkuu wa TASWA na atakuwa Katibu wa kamati hiyo na Mwani Nyangasa ambaye ni mwanachama.

Kamati hiyo itasimamia mchakato wa marekebisho hayo, kisha utaitishwa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama wote kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo na ni imani ya Kamati ya Utendaji kuwa marekebisho hayo ya Katiba hayatachukua muda mrefu, ili mkutano Mkuu wa TASWA ufanyike kabla ya kumalizika robo ya kwanza ya mwaka 2012.

(B) SEMINA, MAFUNZO MWAKA 2012

Kikao hicho pia kilipanga kuhusiana na masuala mbalimbali ya mafunzo kwa wanachama wake mwaka 2012, ambapo Sekretarieti ya TASWA imepewa jukumu la kuratibu tarehe ya mafunzo yote na italitolea taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili Januari mosi, 2012 kwa kuanzia na mafunzo ya Kanda ya Kaskazini, ambayo awali ilikuwa yafanyike Novemba mwaka huu.

(C) MSIBA WA WANAHABARI

TASWA inatoa pole kutokana na misiba ya wanahabari ambao pia ni wanamichezo Halima Mchuka aliyefariki dunia jana na John Ngahyoma aliyefariki dunia leo.

TASWA imeshtushwa taarifa za vifo hivyo na inatoa pole kwa familia za wafiwa, wanahabari na  wanamichezo wengine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wetu. Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wafiwa. Amin
Imetolewa na:
Amir Mhando
Katibu Mkuu - TASWA
30/12/2012        

JOHN NGAHYOMA WA BBC AFARIKI DUNIA

Marehemu John Ngahyoma akiwa kazini enzi za uhai wake.

Tumepata taarifa kwamba Mwandishi wa Habari mkongwe nchini ambaye alikuwa akifanya kazi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), John Ngahyoma amefariki dunia leo asubuhi.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata, karibu na nyumbani kwa Marehemu Danny Mwakiteleko. Mwenye taarifa zaidi atufahamishe.

Tunaitakia moyo wa subira na Mungu awafariji wanafamilia wa Ngahyoma katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN


Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors' Forum (TEF),
Dar es Salaam -Tanzania.
Cell: +255 - 715 -339090
+255 - 787 - 675555

RAIS KIKWETE ATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MTANGAZAJI WA TBC-TAIFA, HALIMA MCHUKA

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana, kufiatia kifo cha mtangazaji maarufu wa siku nyingi wa  shirika hilo, Halima Mohammed Mchuka ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia leo, Alhamisi, Desemba 29, 2011 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

“Nimepokea kwa huzuni habari za kifo cha Halima Mohammed Mchuka. Nakutumia wewe Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki. Nakuomba, kupitia kwako, uniwasilishie salamu zangu kwa wafanyakazi wenzake katika TBC ambao wamempoteza mwenzao na rafiki yao.” Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema ikimkariri Rais.

“Aidha, nataka kupitia kwako niwatumie salamu zangu za rambirambi wana-familia, ndugu na jamaa wote za marehemu. Wajulishe kuwa niko nao katika wakati huu wa maombolezo na kwamba msiba wao ni msiba wangu pia. Nawaomba wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amen.” amesema Rais.

 Rais amesema kuwa Mchuka ametoa mchango mkubwa katika nyanja ya utangazaji nchini. “Sote tutaendelea kukumbuka weledi wake, uzalendo wake na ujasiri wake katika utangazaji uliomsukuma kuwa Mwanamke wa Kwanza katika Tanzania kutangaza mechi za mpira wa miguu”.

Amesema ni dhahiri kuwa nyanja ya utangazaji imeondokewa na mtu muhimu na namna nzuri zaidi ya kumuenzi  Mchuka ni kwa watangazaji waliobakia kuendelea kuiga mfano wake katika ubora wa utangazaji nchini mwetu.

December 29, 2011

KWA MUDA MFUPI TAYARI VODACOM TANZANIA YAKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 6 ZA WAHANGA WA MAFURIKO KUPITIA KAMPENI YAKE YA "Red Alert"

Vodacom Tanzania inawashukuru wote ambao tayari wameshaonesha upendo wao kupitia kampeni ya “Red Alert” na kufanikisha kukusanywa shilingi 6,284,000/= kati ya December 22, hadi December 27, 2011.

Tunapenda kutoa wito wa kuendelea kuchangia Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko kwani bado wanahitaji misaada yetu,kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.

Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa

*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.

Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili

Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990

Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu

Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea

Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri

Hatua ya 7: Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia

'2011 MWAKA WA HUKUMU KWA VIGOGO WENGI WA RWANDA ICTR'

Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle, Arusha
 
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) inaweza kusherehekea mwisho wa mwaka 2011 kwa kujivuna kutokana na hukumu nzito na nyingi zilizotolewa katika mwaka huo.

Mahakama hiyo imetoa jumla ya hukumu 10 katika ngazi zote mbili za mahakama ya awali na mahakama yake ya Rufaa zenye kuhusisha watu 21, akiwemo mwanamke pekee kuwahi kushitakiwa na mahakama hiyo, Pauline Nyiramasuhuko na mtu anayesadikiwa kuwa mpangaji mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, Kanali Theoneste Bagosora.  

Hukumu za ICTR 2011

Gatete ahukumiwa kifungo cha maisha: Machi 29, 2011, ICTR ilianza mwaka mpya kwa kutoa hukumu yake ya kwanza katika kesi inayomkabili aliyekuwa afisa mwandamizi wa serikali ya Rwanda, Jean-Baptiste  Gatete ambaye alitiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari na kuteketeza kizazi. Alipewa adhabu ya kifungo cha maisha jela na kesi hiyo sasa iko mahakama ya Rufaa.

Aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ahukumiwa kifungo cha miaka 30: Mei 17, 2011, Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ilitoa hukumu nyingine nzito katika kesi inayohusisha maafisa wanne wa zamani wa jeshi la Rwanda wakiwemo Afisa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo , Jenerali Augustin Bizimungu na Afisa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jenerali Augustin Ndindiliyimana.

Majenerali hao walitiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.Bizimungu alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela huku mwenzake, Ndindiliyimana alipewa adhabu ya muda aliokwisha tumikia akiwa kizuizini tangu mwaka 2000.Aliachiwa huru mara moja.

Maafisa wengine waliotiwa hatiani ni pamoja na Mkuu wa Bataliani ya Usalama Jeshini, Meja Francois-Xavier Nzuwonemeye na Kapteni Innocent Sagahutu pia wa Bataliani hiyo ambao walipewa kila mmoja wao adhabu za vifungo vya miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. Pande zote mbili za mwendesha mashitaka na utetezi zimekata rufaa.

Mwanamke pekee na wengine watano watiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari: Juni 24, 2011 ilikuwa siku ya pekee katika historia ya ICTR kwa kutoa hukumu ya kesi iliyokuwa na watuhumiwa wengi zaidi kuliko kesi yoyote katika mahakama hiyo.
 
Kesi hiyo maarufu kwa jina la Kesi ya Butare, inajumuisha watuhumiwa sita akiwemo mwanamke pekee, Pauline Nyiramasuhuko, Waziri wa zamani wa Familia na Masuala ya Wanawake na mtoto wake wa kiume, Arsene Shalom Ntahobali. Wawili hao walihukumiwa vifungo vya maisha jela baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu ukiwemo ubakaji na kuteketeza kizazi na uhalifu wa kivita.

Wengine waliotiwa hatiani katika kesi hiyo ni pamoja na Eli Ndayambaje, aliyehukumiwa pia kifungo cha maisha jela, Alphonse Nteziryayo, alipewa adhabu ya kifungo cha miaka 30, Sylvain Nsabimana atatumikia miaka 25 jela ambapo Joseph Kanyabashi alipewa adhabu ya miaka 35 jela. Wote sita wanasubiri tarehe ya kusikilizwa kwa rufaa zao.

Mawaziri wawili waachiwa huru na wengine wawili watiwa hatiani: Septemba 30, 2011, hukumu nyingine ilitolewa katika kesi inayohusisha mawaziri wanne wa zamani wa Rwanda katika serikali ya mpito ya mwaka 1994. Mahakama iliwaachia huru mawaziri wawili ikiwa ni pamoja na Casimir Bizimungu (Afya) na Jerome Bicamumpka (Mambo ya Nje). 
 
Waliotiwa hatiani ni Justin Mugenzi (Biashara) na Prosper Mugiraneza (Utumishi wa Umma) ambao kila mmoja wao alipewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kula njama za kufanya mauaji ya kimbari na uchohezi.Kama ilivyokuwa kwa wote waliotiwa hatiani nao wamekata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Meya wa zamani ahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela: Novemba 17, 2011 Mahakama pia ilitoa hukumu nyingine katika kesi ya meya wa zamani nchini Rwanda, Gregoire Ndahimana. Alitiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari na ukatili dhidi ya binadamu na kuhukumiwa adhabu ya kifungio cha miaka 15. Anasubiri kupangiwa tarehe ya kusikilizwa rufaa yake.

Wanasiasa vigogo wawili wa Rwanda kutumikia jela maisha: Desemba 21, 2011 ICTR ilitoa hukumu ya mwisho kwa mwaka huu katika kesi ya wanasiasa wawili wa kilichokuwa chama tawala cha MRND wakati wa mauaji ya kimbari ikiwa ni pamoja na Rais wa chama hicho Mathieu Ngirumpatse na Makamu wake, Edouard Karemera.Walitiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. Walipatikana na hatia hususa ni kwa sababu ya nafasi yao kama viongozi wa juu wa chama hicho kwa kushindwa kuwazuia wala kuwaadhibu wanamgambo wa chama chao maarufu kama Interahamwe waliokuwa wanashiriki katika mauaji ya kimbari.

Hukumu za Mahakama ya Rufaa    

Luteni Kanali Muvunyi kuendelea kutumikia miaka 15 jela: Aprili 1, 2011, Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya ICTR, ilithibitisha adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela aliyopewa afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda Luteni Kanali Tharcisse Muvunyi. Afisa huyo aliyekuwa katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi Wasiokuwa na Kamisheni (ESO) alitiwa hatiani kwa uchochezi wa mauaji ya kimbari katika hotuba yake aliyoitoa Kusini mwa Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Luteni Kanali Setako kuendelea kutumikia miaka 25 jela:  Septemba 28, 2011 Mahakama ya Rufaa pia ilithitisha adhabu ya kifungo cha miaka 25 jela aliyopewa aliyekuwa afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda, Luteni Kanali Ephrem Setako baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Maafisa wawili waandamizi wa zamani wa jeshi wanusurika vifungo vya maisha: Desemba 14, 2011, Mahakama ya Rufaa ilipunguza hadi miaka 35 jela adhabu ya kifungo cha maisha aliyopewa mtu anayesadikiwa kuwa alikuwa mpangaji mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Kanali Theoneste Bagosora baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari,uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. 
 
Katika mahakama hiyo pia tarehe hiyohiyo ilimpunguzia afisa mwingine adhabu kama hiyo ya kifungo cha maisha jela hadi miaka 15, afisa mwingine wa jeshi, Luteni Kanali Anatole Nsengiyumva. Kwa kuzingatia muda aliokwishatumikia akiwa kizuizini tangu atiwe mbaroni, mahakama iliamuru kuachiwa huru mara moja.  

Kesi ya mtuhumiwa wa ICTR kusikilizwa Rwanda kwa mara ya kwanza: Desemba 16, 2011, Mahakama ya Rufaa ilitoa uamuzi wa kihistoria kwa kuruhusu kesi ya mchungaji Jean Uwikinkindi kwenda kusikilizwa nchini Rwanda.Mahakama mapema ilitupilia mbali rufaa ya mtuhumiwa huyo kupinga uamuzi wa mahakama ya awali ulioamuru kesi hiyo kwenda kusikilizwa nchini Rwanda Juni 28, 2011. Umuazi huo unafungua njia kwa kesi nyingine za watuhumiwa wa ICTR kupelekwa kusikilizwa nchini Rwanda.

Matukio mengine muhimu ICTR


Uchaguzi wa Rais na Makamu wake ICTR: Jaji mwanamke, raia wa Pakistani, Khalida Rachid Khan alichanguliwa kuwa Rais wa ICTR,kuanzia Mei 27, 2011 kwa kipindi cha miaka miwili. Jaji Khan ambaye alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama namba III alikuwa Makamu wa Rais wa ICTR tangu Mei 29, 2007. Wakati hohuo, Rais huyo alitangaza Agosti 24, 2011 kwamba Jaji Vagn Joenson kutoka Denmark aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa ICTR. Jaji huyo alianza rasmi kazi hiyo Agosti 26, 2011.

 Kuachiwa mapema mfungwa wa mauaji ya kimbari: Mfungwa wa mauaji ya kimbari, Michel Bagaragaza, aliachiwa toka gerezani nchini Sweden alikokuwa anatumikia adhabu ya kifungo cha miaka nane jela baada ya kutumikia tayari theluthi mbili ya adhabu hiyo iliyotolewa na ICTR kwa kula njama za kufanya mauaji ya kimbari. Hii ni mara ya kwanza kwa Mahakama hiyo ya Umoja wa Mtaifa kuruhusu mmoja wa wafungwa wake kutoka jela kabla ya muda wa adhabu uliotolewa kumalizika. Bagaragaza alikuwa Mkuu wa Mamlaka ya Chai nchini Rwanda.

Wito kwa mataifa kupokea wanaoachiwa huru ICTR: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi wanachama wa umoja huo kuwapokea watuhumiwa wanaoachiwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na kuendelea kubaki chini ya uangalizi wa mahakama hiyo. Wapo watuhumiwa watano waliokwishaachiwa huru lakini bado wanatafuta nchi za kuwapokea.

TAARIFA KWA WAPIGA PICHA ZA HABARI WOTE TANZANIA

Kwa niaba ya Uongozi wote wa PPAT, napenda kuchukua fursa hii kumpa pole Mpigapicha za Habari Mwenzetu Robert Okanda wa Magazeti ya Daily News na Habari Leo kwa athari kubwa iliyompata kufuatia mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

PPAT ipo pamoja nae katika kipindi hiki kigumu cha kurejesha hali ya makazi, na mali zake katika hali sahihi ya awali.

Kwa taarifa hii PPAT inaomba yeyote atakae kuguswa na tatizo hili la mwenzetu kumchangia chochote alichonachonacho iwe ni mali au fedha, na awasilishe mchango wake huo kwa Mwanakombo Jumaa pale Idara ya Habari Maelezo (Mhazini Msaidizi) au waliyo na M Pesa na Tigo Pesa wazitume 0717002303 au 0755 373999 (Mroki Mroki).

Natanguliza shukrani zetu za thati.
Mroki Mroki
Katibu Mkuu-PPAT

Mtangazaji wa TBC -Taifa, Halima Mchuka afariki Dunia

Halima Mchuka (kushoto) enzi za uhai wake.
MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa  Redio Tanzania Dar es Salaam RTD  na baadae Shirika  la  Utangazaji  Tanzania (SHIUTA) amefariki Dunia. 

Taarifa zilizopatikana  hivi  punde zinadai  kuwa Mtangazaji  huyo  ambaye  alikuwa na  kipaji  kikubwa cha  utangazaji amefariki  Usiku  huu  wa  leo  tarehe  29-12-2011 saa 9.00alfajiri  kutokana  na kupatwa  na  stroke ya  ghafla  .
 
“Alikuwa  na tatizo  hilo  jana mchana mara baada  ya kutangaza kipindi  cha salaam cha  TBC-Taifa na akazidiwa ndipo  alipopelekwa  Hospitali  na sasa  ndiyo amefariki  dunia.”alibainisha mmoja wa watangazaji wa TBC ambaye  alikuwa jirani  na mtangazji  huyu.

 Halima Mchuka inaaminika  kuwa  alijiunga  na Radio  Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi  katika idara ya  Habari na idara   ya Mipango.

Wadau  wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili  kwa  kuwa  mwanamke wa awali  kuangaza mpira  katika  ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki  na  Kati.

“Unapotaja mpira wa miguu wakai huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu  dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wachezaji nguli wa  Tanzania wa wakati huo.

Kwa hakika  si  wasikilizaji  wa  RTD na wanamichezo tu  bali  ata  watu wa Karibu  ambao  waliwahi  kufanya nae  kazi     tunamtazama kuwa  ni  mtu mpole  mwenye  huruma  na  kusaidia  wenzake pale  penye tatizo  ambalo  yeye  anaweza kulitatua.

”unajua  huyu  mama  mimi ndiye aliyenisaidia  kuweza kupata  kazi  kwenye taasisi  hii  nilikuwa wala  simfahamu  mtu ,amenisaidia sana.”kuficha  ni  dhambi  alinidokeza mfanyakazi mmoja wa SHIUTA.

Mara  ya  mwisho kuongea  na  mwana mama  huyu nilikuwa nikiwa Iringa alinipigia simu na kuniulizia taarifa  za  familia  yangu  na kuniambia  nimtunze sana  mtoto  wangu  lakini   huku akiniambia  na kutambua “ mbona leo unaongea  kwa unyonge” ah “ Halima  hapana  ila nipo  eneo  ambalo  watu  wanasoma ndiyo  maana  naongea  kwa sauti ya  chini “nilimjibu wakati huo  kwani nilikuwa makaba ya  Chuo Kikuu  cha  Tumaini Makumira- Iringa.
 
Mungu  ailaze Roho ya Bi. Halima Mchuka pahala pema peponi Amina

Kibanda ajiengua Kamati ya Kutafuta Vazi la Taifa

Mhariri Mtendaji Free Media Ltd na Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
UTANGULIZI

Itakumbukwa kwamba Desemba 15 mwaka huu, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi aliniteua kuwa mjumbe katika Kamati ya Kitaifa ya Kukamilisha Mchakato wa Kupata Vazi la Taifa.

Siku chache baada ya uteuzi huo, nilipokea wito wa kuitwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi kutokana na makala ambayo ilichapishwa katika gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 30 mwaka 2011.

Kufuatia mahojiano hayo, Desemba 21 nilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako polisi na wanasheria wa serikali walinifungulia mashtaka ya kuwachochea askari kutoitii Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nilipata dhamana katika kesi hiyo ambayo imeahirishwa hadi Januari 19, 2012 itakapotajwa tena.

MSIMAMO NA UAMUZI WANGU

Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu uteuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo sambamba na uamuzi wa serikali kunihoji na kunifungulia mashitaka, busara yangu binafsi na kwa kuzingatia ushauri nilioupata kutoka kwa wahariri wenzangu, nimefikia uamuzi wa kujitoa katika Kamati ya Kutafuta Vazi la Taifa.

Nimelazimika kufikia uamuzi huo kwa sababu zifuatazo:

1. Mosi, uamuzi wa serikali kupitia Jeshi la Polisi na Waendesha Mashitaka kunifungulia kesi ya kuchochea uasi inanifanya niamini kwa dhati kwamba, haina imani nami binafsi na ina nia ya dhati ya kuhakikisha ninaadhibiwa na hivyo kukinzana na imani ambayo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameionyesha kwangu kupitia uteuzi wake.

2. Pili, nimelazimika kufikia uamuzi huo wa kujitoa katika kamati hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na kufunguliwa mashitaka na polisi na hatimaye kufikishwa kwangu mahakamani usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo inaongozwa na Waziri Nchimbi.

3. Tatu, kwa kuyatambua hayo nimeona itakuwa ni uamuzi wenye hekima kujitoa katika kamati hiyo kwa kuzingatia uhalisia kwamba nitashindwa kutimiza wajibu wangu ipasavyo nikiwa mjumbe katika kamati hiyo, sababu kubwa ikiwa ni kuwapo kwa hali ya kutoaminiana na kutiliana shaka kati ya wizara na waziri Nchimbi kwa upande mmoja na mimi mteule katika kamati huyo kwa upande mwingine.

4. Mwisho, wakati nikichukua uamuzi huo mgumu, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Waziri Nchimbi kwa kuonyesha imani nami hata kuniteua kuwa miongoni mwa wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Kitaifa ya Vazi la Taifa.

Imetolewa na:
Absalom Kibanda
Mhariri Mtendaji Free Media Ltd na Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri

SUPER D BOXING COACH AJIVUNIA MAFANIKIO 2011

Rajab Mhamila 'Super D'
Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti na mkoa wa  Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wa ngumi katika kipindi cha mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha  alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.

Alisema pamoja na hilo pia ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.

Katika hatua nyingine Super D amekua akitoa  mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali  kwa njia ya DVD zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya
utangulizi.

Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua mabondia wengine chipkizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa vipaji vyao.

Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga  Mustapha Doto,kwa pointi 60-57 alishinda  ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward lililofanyika Desemba 25 mwaka huu.

United States Provides 80 Million Tanzanian Shillings in Disaster Relief to Tanzanian Flood Victims

Ambassador Alfonso E. Lenhardt (left) and Tanzania Red Cross Society Secretary General, Adam Kimbisa during the handover ceremony.
U.S. Ambassador to The United Republic of Tanzania Alfonso E. Lenhardt announced on December 24 that the American people have provided disaster relief funds to flood victims in the Dar es Salaam Region.  Relief supplies totaling USD $50,000 (approximately TSH 80 million) are being made available through the United States Agency for International Development Office of Foreign Disaster Relief (USAID/OFDA) to the Tanzanian Red Cross Society to support families and communities affected by the floods.

Dar es Salaam is currently experiencing devastating floods resulting from the heaviest rainfall in 55 years according to the Tanzania Meteorological Agency.  A rapid assessment by the Tanzanian Red Cross estimates the total number of people affected by the floods over 50,000 (approximately 10,000 families); to date about 10,000 people (approximately 2,000 families) have been displaced and are being accommodated in temporary displacement/holding centers.  Over 200 people have been injured, with approximately 2,500 people missing, mostly children, and 23 people have been confirmed dead, and the toll is expected to rise in coming days. 

Ambassador Lenhardt handed over the funds to Secretary General of the Tanzania Red Cross Society Adam O. Kimbisa on the morning of December 24.  During the check handover, Ambassador Lenhardt said, "the $50,000 USD in disaster assistance from the American people will be used for immediate relief to 10,000 affected families with non-food items including blankets, buckets for water storage, mosquito nets, and water treatment tabs as well as shelter items, including family tents, tarpaulin, and sheeting.

Secretary General Kimbisa was joined by Joseph S. Kimaryo, Director, Disaster Management & Logistics, and Stella Marealle, Information and Dissemination Manager for the Tanzanian Red Cross Society.

This is the third time in 2011 the US has provided rapid disaster relief to Tanzania; including $50,000 in relief for the ammunitions explosion in Ilala district in February as well as donating medical supplies to Mnazi Moja Hospital in Zanzibar after the Zanzibar ferry accident in September.

The record rainfall, which began on December 20, worsened an already disastrous situation has caused significant damage to key infrastructure including bridges and roads connecting the suburbs and the city center.  Public transport has been brought to a near standstill.  Many houses in lowland areas have been completely destroyed, leaving thousands displaced.  A significant number of wells which serve as major sources of water for family use have been over-flooded causing families to go without clean and safe water. 

CHUNGA SANA MLIO WA SIMU YAKO

TUSIPOKUWA MAKINI YATATUPATA HAYA.....
KOSA LA KWANZA SIMU KUITA/KUWA NA MLIO AU KUTOZIMWA KATIKA NYUMBA YA IBADA
 KOSA LA PILI MLIO WENYEWE SIO SAHIHI MAHALI HAPO....
KOSA LA TATU UNASUMBUA WENZIO.....

KOSA LA NNE..............................
Na Imma
Kwa hisani ya Mjengwa Blog

December 28, 2011

Korea Kaskazini yafanya maziko ya Kim Jong -il

Jeneza la Kim Jong il
Korea Kaskazini inafanya maziko ya kitaifa ya kiongozi wake Kim Jong-il huku msafara mkubwa wa magari yaliyosindikiza jeneza la kiongozi huyo ukipitia mji mkuu Pyongyang.

Picha za runinga zimeonyesha maelfu ya wanajeshi wakitoa heshima za mwisho kwa picha ya kiongozi huyo iliyopitia kwenye barabara za mji.

Mridhi wa uwongozi ambaye ni mwanawe wa kiume Kim Jong-Un amezindikisha jeneza la babake lililokuwa juu la gari maalum. Kim Jong-il alifariki dunia Decemba 17 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa na miaka 69.

Hakuna viongozi wa nje walioalikwa wala waandishi wa habari wa kimataifa. Wadadisi wanasema mazishi ya leo ni sambamba na ya mwasisi wa nchi hiyo Kim IL-Sung mwaka 1994 yalioandamana na gwaride kubwa ya kijeshi.

Kiongozi mtarajiwa Kim Jon-Un ameandamana na mjombake Chang Song-taek anayetarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uwongozi mpya pia mkuu wa jeshi Ri Yong-ho, alionekana kando ya jeneza la Kim Jong-Il.

Kabla ya kufariki kiongozi wa Korea Kaskazini alikuwa katika mchakato wa kumtayarisha mwanawe Kim Jong-Un kuchukua hatamu za uwongozi. Kifo chake cha ghafla cha Kim Jong Il kimepelekea hofu ya kuzuka mzozo wa uwongozi katika taifa hilo lenye msingi wa ujamaa.
Source:BBC

December 27, 2011

Mgogoro wa CUF




Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohammed akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kutoa tamko kuhusu pingamizi la kukataa kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Chama ya chama hicho.

CCM YASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR, NAPE AKABIDHI VYAKULA VYA SH. MILIONI NNE.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikabidhi msaada wa vyakula kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik , katika ofisi ya mkuu huo jana. Vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 4, vimetolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia waliokumbwa na maafa ya kafuriko yaliyosababishwa na vyua katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye akizungumza na kina mama wenye watoto, ambao aliwakuta kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  alipokwenda kutoa msaada wa CCM wa vyakula kwa waliopatawa na mafuriko. Kina mama hao, Mariam Msimbi na Asha Selemani (kulia) walifika kwenye ofisi hiyo kutafuta ufumbyuzi wa ndoa zao ambapo wamedai wametorokwa na waume zao huku wakiwa na watoto wadogo.

Nape akizungumza na baadhi ya wananchi alipofika kwenye kambi maalum ya Mchikichini walikohifadhiwa waathiorika mwa mafuriko, wilayani Ilala.

Nape(katikati) akikagua eneo la shule la Msingi Mchikichini ambako wamehifadhiwa waathirika wa mafuriko wilayani Ilala

Nape akipata taarifa za matibabu wanayopatiwa waathirika wa mafuriko, katika kituo cha muda cha wathirika hao, shule ya msingi Mchikichini.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikabidhi msaada wa vyakula kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik , katika ofisi ya mkuu huo jana. Vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 4, vimetolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia waliokumbwa na maafa ya kafuriko yaliyosababishwa na vyua katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Nape akimchumu mtoto Fatuma Fadhili aliyekuwa na mama yake Ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Serengeti Breweries Limited (SBL) yazindua Senator Extra Lager

Ni kitu kipya katika soko kinatambulishwa kwenu na kampuni ya Serengeti Breweries Limited ndani ya jiji la Mwanza, Kitu kinaitwa Senatar Extra Lager Bia ina alkohol 6 mwanawane.


Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Ephraim Mafuru akizungumza katika uzinduzi wa bia mpya ya Senator Extra Lager ambayo imeanza kuzaliashwa na kusambazwa na kampuni hiyo. Bia hiyo inawalenga wachapakazi wa hali ya chini kabisa, wakulima, wavuvi na wengineo wa kanda ya ziwa na majirani zake. Bia ya Senetor itauzwa kwa bei nzuri ya shilingi elfu moja na mia tatu tu (1,300/-)

Watumishi wa SBL, mawakala na wadau wa kampuni hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru wakati wa uzinduzi wa bia ya Senator Extra Lager Jijini Mwanza.
                                           *********************************************
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kinywaji kipya cha bia ya Senator, kinachozalishwa kwa kutokana na mazao ya mtama na shayiri na kuwataka wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kulima mazao hayo kwa vile watakuwa na soko la uhakika.

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika katika kiwanda cha SBL Mwanza hivi karibuni na kuhudhuruiwa na baadhi ya wafanyakazi,mawakala na wauzaji wa bidhaa za kampuni ya SBL. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kinywaji hicho kipya, Mkurugenzi wa Masoko wa (SBL) Ephraim Mafuru,alisema serikali inawaunga mkono kwa kusisitiza wakulima kuchangamkia kilimo cha mazao ya mtama na shayiri.

Alisema kuwa wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wanapaswa kuanzisha kilimo cha mtama na kuuza mazao yao katika kiwanda cha SBL kinachozalisha kinywaji hicho na watakuwa na soko la uhakika.

“Tunaagiza malighafi kutoka nje ya nchi kwa asilimia 80 ili kukidhi mahitaji kwa sababu asilimia 20 ya malighafi ya hapa nchini ni ndogo,hivyo wakulima wa Kanda ya Ziwa wanapaswa kulima na kuuza mazao yao kiwandani kwetu na wao kunywa kinywaji hiki cha Semator ili kusukuma biashara hii.Soko la mazao yao kama mtamama na mahindi linapatikana SBL ambapo tumekuwa tukinunua kilo moja ya mtama kwa shilingi 600,”alisema Mafuru.

Alisema kuwa bia ya Senator yenye kilevi cha asilimia 6 inazalishwa kutokana na kimea cheupe kinachotokana na mtama, kinywaji ambacho kimemlenga mtanzania wa kipato cha kawaida wa mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 
Alieleza kuwa kinywaji hicho tayari kipo sokoni na kuwataka wateja wake ambao ni wavuvi na wakulima kukinunua ambapo bei ya mlaji itakuwa ni shilingi 1300,ambapo Januari mwakani watafanya matamasha ya kukitangaza kinywaji hicho zaidi katika maeneo ya vijijini.

Aidha alisema kauli mbiu ya kinywaji hicho ni ‘bia ya wachapakazi ahsante kwa kutuwezesha kuwa kampuni kubwa’ ambapo SBL inatarajia kudhamini ngoma za utamaduni za makabila ya Wasukuma za Wagika na Wagalu. 
 
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa SBL Kanda ya Ziwa, Stansaus Theophile, alisema bei tishari moja ilenye chupa 25 liytauzwa kwa bei ya shilingi 25 kwa mawakala,shilingi 25,400 (mawakala wa kati) na shilingi 26,000 kwa mawakala wadogo na mlaji shilingi 1300.

WAKAZI WA KARIAKOO ZILIZOKUA KOTA ZA BANDARI WAPINGA KUHAMISHWA WALA KUVUNJIWA NYUMBA ZAO

Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania.(Picha na Mpigapicha Wetu)

Baadhi ya wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani wakimsikiliza mwanasheria wao Dkt. Sengondo Mvungi kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania.(Picha na Mpigapicha Wetu)
                                              *********************************************
Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Kariakoo Kota za Bandari kata ya Gerezani wameitaka serikali kutowahamisha wala kuwavunjia nyumba zao hadi hapo kesi yao iliyopo mahakama kuu kitengo cha Ardhi itakapo kamilika.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa mtaa huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa nyumba hizo walinunua kutoka serikali na kupewa mkataba.

Alisema eneo hilo linataka kuchukuliwa na serikali ili kujenga kituo cha mabasi yaendayo kasi bila ya kujali kuwa nyumba hizo waliuziwa ambapo serikali iliingia mkataba na mtu mmoja mmoja.

"Tumesikia fununu kuwa serikali inataka kuja kuvunja nyumba zetu kinguvu ikiwa kesi bado ipo mahakamani",alisema

Kwa upande wake katibu mwenezi wa siasa wa chama cha Mapinduzi Bw.Akida Hafidhi alisema serikali ilifanya makosa kuingia katika eneo hilo ikiwa inajua kabisa kuna mgogoro na kuongeza kuwa wanaomba haki iweze kutendeka kwa kuiachia mahakama kutoa maamuzi kama katiba inavyoelekeza.

Alisema serikali inatakiwa kutambua kuwa wakazi wa eneo hilo wanamiliki nyumba hizo kimkataba na hakuna mtu aliyevunja mkataba huo ambapo walinunua kutoka kwao.

Hata hivyo walisema watashangazwa endapo watasikia kuwa kuna mtu anaingilia uhuru wa mahakama ikiwa ibara ya 4(1) na 107(a) ya katiba ya Tanzania inaeleza wazi kuwa chombo cha mwisho chenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ni mahakama ya Tanzania.

"Tumesema hivyo kwa sababu tulisikia baadhi ya watendaji serikalini walisema tulienda mahakamani kimakosa huku wakijua dhahili kuwa ni mahala ambapo haki inapatika",walisema

Walisema wanamuomba Rais Jakaya Kiwete asije akadanganywa kwa hilo kuwa kuna makubaliano yaliofanyika huku wakisisitiza kuwa kesi iliyopo ni kuvunjwa kwa mkataba na sio madai ya fidia kama ambavyo baadhi wa watendaji walivyopeleka taarifa serikalini.