Tangazo

December 18, 2011

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI, AKABIDHI NISHANI YA DR. WILBERT CHAGULA JIJINI KAMPALA

Rais Jakaya Kikwete akiwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib Bilal na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mara baada ya kurejea jijjini Dar es salaam jana kutoka Kampala, Uganda, alikohudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu.

Rais Jakaya Kikwete akiagwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mh Nsavike G.  Ndatta katika uwanja wa ndege wa Entebbe jana Desemba 17, 2011 asubuhi wakati akiondoka Uganda kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu.

Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Bw. Clement A. Chagula na bintiye Olivia A. Chagula medali kwa niaba ya baba na babu yao Marehemu Dkt. Wilbert Chagula, ambaye aikuwa ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza na mmoja wa  watu maarufu waliotunukiwa nishani katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Bw Chagula, ambaye ni mtoto wa marehemu, hakuweza kufika Dar es salaam kupokea medali hiyo na Rais alipokuwa Kampala akatumia nafasi hiyo kumpatia leo asubuhi katika hoteli ya Speke Commonwealth Resort. PICHA/IKULU

No comments: