Tangazo

March 20, 2012

Sherehe za kuzaliwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Mkewe Mama Sitti Mwinyi (katikati) wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa (kulia) kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo,Muhashamu Salitaris Melchior Libena iliyofanyika leo Ifakara,Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akihutubia kwenye Sherehe hizo.

Mh. Lowassa akibadirishana mawazo na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea.

Mh. Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi wa Jimbo jipya la Kanisa Katoliki Ifakara.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo mara baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika leo Ifakara,Mkoani Morogoro.

No comments: