Tangazo

April 11, 2012

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AZINDUA CHUO CHA VETA MKOA WA LINDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim, wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufe, kuashiria uzinduzi rasmi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA baada ya kuzindua rasmi chuo hicho kilichojengwa Mkoa wa Lindi. Uzinduzi huo ulifanyika jana Aprili 10, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa, Balozi wa Korea nchini, Young-Hoon Kim na Viongozi wa VETA, wakati akitembelea na kukagua baadhi ya majengo mapya yaliyojengwa ya Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA, baada ya kuzindua rasmi chuo hicho mkoa wa Lindi jana Aprili 10, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: