Tangazo

May 3, 2012

Program ya Kufundisha Kiswahili yazinduliwa Chuo Kikuu Indiana: Serikali ya Marekani kuanza kufadhili wanafunzi wa Kimarekani kujifunza Kiswahili

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar (wa pili kulia), akiwa kwenye mazungumzo na Wakuu wa Programu za lungha za Kichina, Kiswahili na Kituruki Chuoni Indiana wakati wa ziara yake chuoni hapo kuzindua Porgramu ya Kiswahili tarehe 1.5.2012.

Balozi Maajar (kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa masomo wa Chuo Kikuu cha Indiana tarehe 1.5.2012 alipotembelea chuoni hapo kuzindua program ya Kiswahili. Kutoka Kushoto ni Balozi Maajar, Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi Larry Singell na msaidizi wake Maria Bucur-Deckard (wa mwisho kulia) na Mratibu wa Programu ya Kiswahili Erick Amick.

Wanafunzi wanaosoma program ya Kiswahili chuoni hapo wakijiandaa kula chakula cha mchana na Balozi Maajar. Wanafunzi hao wataenda Zanzibar mwezi Juni mwaka huu kwa muda wa mwaka mmoja kama sehemu ya program hiyo ya kujifunza Kiswahili.
Balozi Maajar kwenye picha na walimu wa Programu ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Indiana Profesa Alwiya Omar na Mwalimu Deo Tungaraza.

Balozi Maajar (kushoto), akizungumza na Mtanzania ambaye pia anafundisha Chuoni hapo Idara ya Sayansi ya Jiolojia Bw. Jackson Njau (katikati), na Bw. Thompson waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa program hiyo ya Kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Indiana tarehe 2.5.2012.

Balozi Maajar kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliojiunga na progamu ya Kiswahili na wengine waliomaliza kozi zao za masomo chuoni hapo ambao walichukua somo la Kiswahili pia.
Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Indiana Bw. Patrick O’Merara akimkaribisha Balozi Maajar kuhutubia kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na uongozi wa Chuo hicho kuzindua rasmi program hiyo ya Kiswahili tarehe 1.5.2012.


Balozi Mwanaidi Maajar akihutubia kwenye hafla ya kusindua porgramu ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Indiana nchini Marekani tarehe 1.5.2012. Programu hii ya kufundisha lugha ya Kiswahili ni ya kwanza nchini Marekani inayopata ufadhili wa Serikali Kuu ya Marekani.

Balozi Maajar akipongezwa na Makamu wa Rais wa Chuo cha Indiana Bw. Patrick O’Meara, mara baada ya kumaliza hotuba yake iliyoelezea historia ya Kiswahili nchini Tanzania na kazi kubwa iliyofanyika ya kukuza Kiswahili na kuunganisha Taifa. Hotuba hii ilipokelewa vizuri sana ambapo pia ilielezea pia ilielezea umuhimu wa wanafunzi wa Kimarekani kujifunza Kiswahili. Pichani umati wa wageni wakimsindikiza Balozi Maajar kwa makofi huku wamesimama.


No comments: