Tangazo

May 22, 2012

TBL YAMZAWADIA GARI NA BAJAJ WAKALA BORA TANZANIA

Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Kusini ya Mbali,  James Kavuma (katikati), akimkabidhi ufunguo wa Bajaj, Augustine Kisinja baada ya kushinda uwakala bora wa bia za TBL nchini katika hafla iliyofanyika mjini Makambako, mkoani Njombe hivi karibuni. Pia Kisinja alizawadiwa gari aina ya Jac Canter lenye thamani ya sh. milioni 47.

James Kavuma (kulia) wa TBL, akipongezwa na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo kwa kampuni hiyo kuwafthamini wafanyabiashara wa bidhaa zao.

Mfanyabiashara Augustine Kisinja ambaye ameshinda uwakala bora Tanzania kwa kuwa muuzaji na msambazaji mzuri wa vinywaji vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akiendesha Bajaj yyenye thamani ya sh. mil. 4.7 aliyozawadiwa na kampuni hiyo hivi karibuni mjini Makambako, Njombe. Pia Kisinja alizawadiwa gari aina ya Jac Canter lenye thamani ya sh. milioni 47.
 

Augustine Kisinga (kulia) akizungumza na James Kavuma wa TBL, baada ya kuzawadiwa gari na Bajaj.

 Meneja wa Kampuni ya bia TBL kanda ya Kusini, James Kavuma, (aliyekaa kulia) akiwa na mshindi wa Gari na Bajaj Bw. Augustine Kisinja, katika picha ya pamoja na wafanyakazi wake wakati wa makabidhiano hayo katika mji wa Makambako.

No comments: