Tangazo

June 22, 2012

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAZINGIRA ENDELEVU JIJINI RIO DE JANEIRO-BRAZIL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika Ukumbi wa mkutano, wakati walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Balozi Liberata Mulamula (kulia), akifurahia jambo baada ya kukutana na Wabunge wa Tanzania, Mbunge wa Kahama, Bw. James Lembeli, (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (katikati),  Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu, katika Viwanja vya Kumbi za mikutano ya Rio+20.

No comments: