Tangazo

June 20, 2012

Pambano la Bondia Miyeyusho layeyuka


Pambano la masumbwi kati ya bondia Francis Miyeyusho na  mmalawi John Massamba lililokuwa lifanyike ijumaa, limeahirishwa mpaka hapo tarehe itakapotajwa tena kuwa Miyayusho atacheza na nani, lini na wapi.

Haya yamekuja kutokana na bondia John Masamba toka Malawi akiwa hana hadhi ya kucheza na Miyeyusho na lkuwa wasiwasi wa afya yake.

Bondia huyo toka Malawi mwenye rekodi ya mapambano ya kupigwa mawili na kushinda mawili, amecheza mwaka 1969, inaonekana ni mbovu na rekodi yake ya utata ukilinganisha na miyeyusho mwenye mapambano 42 ya kueleweka.

Kutokana na utata huo wa bondia wa Malawi na kutokamilisha malipo na  vibali vyote toka Utamaduni na michezo, hivyo mpambano umesitishwa mpaka taratibu zitakapokamilika za upande wa vibali na  kumleta bondia mzuri wa kucheza na Francis Miyeyusho.

Mapambano mengine yatakuwepo kama kawaida katika ukumbi wa Dar Live kati ya Francis Cheka na Jafet Kaseba.

No comments: